MKUU WA WILAYA YA ARUSHA AGOMEA MABWENI AAGIZA TAKUKURU WACHUNGUZE UBADHIRIFU WA FEDHA ZA SERIKALI | Tarimo Blog


Mkuu wa Wilaya ya Arusha akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Arusha amegomea ujenzi wa mabweni katika shule ya Sekondari Corona ambayo yamegharimu shilingi Milioni  160 na hayajakamilika.

Mkuu wa Wilaya Amesema Takukuru wachunguze ujenzi huo na hatua zichukuliwe kwa wahusika watakaobainika wamehujumu fedha za Serikali.

Pia Mkuu wa Wilaya ameagiza utaratibu unaotolewa na Tamisemi uzingatiwe katika usimamizi wa fedha za miradi ya shule pia Kamati za shule zihusishwe.

Mkuu wa Wilaya ameonya baadhi ya watumishi wa idara ya Elimu kuingilia Kamati za ujenzi za shule kinyume na utaratibu wa serikali.

Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya Amesema watu wanaohusika na manunuzi lazima wajitathimini la sivyo watachukuliwa hatua kali za Kisheria endapo itabainika wamefanya kinyume na utaratibu.

Pia Mkuu wa Wilaya amesema wakuu wa shule watoe taarifa kwa Serikali endapo utaratibu unakiukwa kwani tatizo likitokea Hawatobaki salama.

Mwisho mkuu wa Wilaya amesisitiza watumishi wa Serikali kuwa macho na fedha za Serikali, wasimamie kwa uadilifu mkubwa.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2