*Jatu kutoa elimu ya kunufaisha watanzania
Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
MISS Tanzania 2018 Queen Elizabeth amekula bingo la Balozi wa JATU Plc kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa ajili kuzungumza na vyuo vikuu (Unitalk).
Akizungumza na waandishi Habari wakati wakimtangaza Balozi huyo Meneja Mkuu wa JATU Plc Mohamed Simbano amesema kuwa kuwa na Balozi ni kutaka kuwaunganisha wanafunzi fursa zilizopo JATU kutokana na kuwepo kwa changamoto ya ajira.
Simbano amesema kuwa wanafunzi wanaposoma wakipata elimu wananweza kuwa wakulima au Wakala na kuweza kujiajiri zaidi kuliko kutegemea kuajiriwa.
Simbano amesema JATU wanafunzi wengi wanapokuwa vyuoni hawana elimu kuja kuishi mtaani hivyo wakipata elimu wanavyohitimu wanaweza kujua sehemu ya kuanzia.
Nae Balozi wa JATU Plc Queen Elizabeth amesema wanafunzi wanachangamoto pindi wanapohitimu wanapoingia katika soko la ajira hivyo JATU itafungua fursa.
Amesema JATU kuingia hakuhitaji kuwa na mtaji mkubwa hivyo hata kwa fedha zao wanaweza kuwa sehemu ya Jatu.
Miss Elizabeth amesema wataanza na vyuo 10 wataendelea kutokana na mahitaji yaliyopo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment