SERIKALI YAJIPANGA KATIKA USIMAMIZI WA UPATIKANAJI WA NGOZI BORA | Tarimo Blog


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi akiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya kufunga mafunzo ya wakaguzi wa Ngozi Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Sekta ya Mifugo) Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza wakati akifunga mafunzo ya wakaguzi wa Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam,Pwani pamoja na Morogoro) yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mdau wa bidhaa ya ngozi akioneshwa namna ngozi inavyotakiwa kuwa na ubora wakati mafunzo ya wakaguzi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel akionesha mfano wa Ngozi inavyotakiwa kuwa katika ubora wake huo.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Mazao ya Mifugo,Usalama wa Chakula na Lishe wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (sekta ya Mifugo) Bw.Gabriel Bura akizungumza na wakaguzi wa Ngozi  Kanda ya Mashariki  wa mkutano huo uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika mafunzo ya Ukaguzi wa Ngozi.

Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv

SERIKALI imesema kuwa ngozi nyingi zimekuwa zinakosa ubora kutokana na kutokuwa na udhibiti hivyo kwa sasa kanuni na sheria zimeboreshwa katika kuongeza mnyororo wa dhamani wa bidhaa hiyo.

Hayo ameseyama katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Mifugo) Profesa Elisante Ole Gabriel wakati akifunga mafunzo ya wakaguzi wa Ngozi wa Kanda ya Mashariki yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Profesa Ole Gabriel amesema ngombe wako milioni 33 na kufanya Tanzania kuwa nchi ya Pili kwa Afrika kuwa na Ng'ombe wengi hivyo bidhaa ya ngozi inatakiwa kuwa na ubora na kuwa na faida ya Ng'ombe.

Amesema nyama inayoliwa kwa Siku moja ni Kilogram Milioni 2.6 sasa kwa kiwango hicho tunahitaji kupata ngozi bora kutokana na kuachana na uchunaji wa Ngozi wa mazoea.

Profesa Ole Gabriel amesema katika viatu milioni 45 vya Ngozi vinavyovaliwa ni viatu vya Ngozi ya ndani milioni 1.4.

"Serikali imedhamiria hivyo wakaguzi msituagushe katika hili kwa mifumo yote ya kupata ngozi bora imewekwa "amesema.

Amesema wachunaji Ngozi wana leseni hivyo na wanatambuliwa kisheria ambapo hatuhitahiji kuwa na ngozi zisizo na ubora.

Profesa Ole Gabriel amesema kuwa halmashauri zihakikishe asilimia 15 ya mapato katika  bidhaa katika mifungo irejeshwe katika Wizara hiyo ili ziweze kutumika katika kuoshea Ng'ombe na mambo kengine.

Amesema kuwa upatikanaji wa Ngozi bora kunatokana na afya bora ya Ng'ombe hali ambayo wafugaji waache ufugaji wa mazoea wa kufanya Ngozi kukosa ubora.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2