*Kamanda Lyanga asema watakwenda kisasa kukabiliana na wahalifu wa Makosa ya Kimtandao
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV Mkuranga
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji limesema kuwa wahalifu wa Makosa ya Kimtandao wa mbinu nyingi lakini Polisi watakwenda kwa mbinu zingine za kisasa.
Hayo aliyasema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji Onesno Lyanga wakati akifungua mafunzo ya Tathimini na ufuatiliaji wa Makosa ya Kimtandao kwa askari Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Rufiji yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki.
Kanda kwa askari wa Makosa ya Kimtandao iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki yaliyofanyika wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Kamanda Lyanga amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwani wahalifu wanambinu nyingi hivyo kukutana na TCRA kunajenga uimara na kufanya kazi hiyo kwa weledi kwa Polisi na kuhudumia wananchi na kutoa elimu kwa kutumia mawasiliano salama.
Lyanga amesema kuwa pale wanapokuwa wamepata taarifa za mwananchi dhidi ya kufanyiwa uhalifu wa kimtandao huo wanachukua hatua za haraka ikiwemo kuwasiliana na watoa huduma za mawasiliano.
Amesema mifumo ya ufatiliaji wa makosa na sheria zimeboreshwa ikiwa ni kumlinda mwananchi katika kupata huduma salama na sio kufanyiwa uhalifu na matapeli.
"Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji tutaendelea kushirikiana na TCRA katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwa ubora kwa kuhakikisha wananchi wanahudumiwa kwa weledi pale taarifa za kufanyiwa utapeli wa Makosa ya Kimtandao zinapopatikana na hiyo ni pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya sheria"amesema Lyanga.
Naye Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa utoaji elimu ni endelevu kwani kadri ya Teknolojia inavyobadilika ndivyo wahalifu wanabuni mbinu zingine ikiwa ni Pamoja na wananchi kuendelea kupata elimu ya mawasiliano.
Amesema kuwa TCRA imejipanga katika kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali katika kwenda sambamba na ukuaji wa Teknolojia ya Mawasiliano kwa Kasi kwa kuweka mifumo ya kuweza kukabiliana na wahalifu.
Mhandisi Odiero amesema wananchi wanatakiwa wanapofika Polisi wanapata huduma kutokana na Polisi kuwa na mafunzo mbalimbali ya kuhusiana na mawasiliano na Pamoja na Makosa ya kimtandao.
Kwa Upande wa Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Mtandao wa Jeshi la Polisi Makao Makuu Joshua Mwangasa amesema kuwa kutokana na elimu Makosa yanapungua kutokana na kuwepo kwa elimu kwa Askari wa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na wahalifu wa Makosa ya Kimtandao.
Amesema uchunguzi wa Makosa ya kimtandao una mambo mengi wakati mwingine yanavuka mipaka ya nchi kupata taarifa.
Amesema kuwa mafunzo waliyoyapata askari watatoa huduma bora kwa wananchi wanapokwenda kutoa taarifa za Makosa ya kimtandao.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment