Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeikabidhi Kampuni mpya ya Afcons mara baada ya kuvunja mkataba wa Mkandarasi wa Mradi wa Maji wa Chalinze kutoka Kampuni ya OIA ya India kwa kushindwa kukabidhi mradi kwa wakati.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Cpyprian Luhemeja ameyasema hayo leo alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maji pamoja na kuzungumza na wafanyakazi wa Dawasa Chalinze na Wami.
Alisema kuwa kwa sasa mradi wa Chalinze awamu ya tatu umepata majibu kwani tayari amepatikana mkandarasi mpya kutoka Kampuni ya Afcons ambaye amepewa miezi nane kukamilisha mradi huo.
Alielezea kuwa mkandarasi huyo alikuwa akiwasumbua kwa muda mrefu kwa kufanya kazi chini ya kiwango na kusababisha wananchi wa Chalinze kukosa huduma ya maji kwa muda mrefu kwani alitakiwa kukamilisha mradi huo mwaka 2017 lakini pamoja na kuongezewa muda alishindwa kukamilisha.
Alimtaka mkandarasi huyo mpya kutoka Kampuni ya Afcons kuhakikisha anatekeleza mradi huo kwa wakati kwani akienda tofauti na makubaliano ya mkataba hatosita kumfukuza kwani wananchi wamechoka kusubiri na kuteseka kwa kukosa huduma ya maji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Cpyprian Luhemeja akitoa maelekezo kuhusu mitambo ya kusukumia maji iliyoletwa na mkandarasi mpya ya Afcons baada ya kusitisha mkataba wa Mkandarasi wa Mradi wa Maji wa Chalinze kutoka Kampuni ya OIA ya India kwa kushindwa kukabidhi mradi kwa wakati.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa Cpyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) ilivyovunja mkataba wa Mkandarasi wa Mradi wa Maji wa Chalinze kutoka Kampuni ya OIA ya India kwa kushindwa kukabidhi mradi kwa wakati na kumpatia mkandarasi mpya ambayo ni kampuni ya Afcons.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment