Katibu wa kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Uratibu wa ujenzi wa mji wa Serikali Meshack Bandawe (aliyenyosha mkono) akikagua ujenzi wa barabara za lami za mji wa Serikali zinazojengwa kwa gharama ya bilioni 88.1 zenye urefu wa 51.2kilomita ambazo zimefikia asilimia 56 ya ujenzi wake Mtumba Jijini Dodoma.
Katibu wa kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Uratibu wa ujenzi wa mji wa Serikali Meshack Bandawe (aliyenyosha mkono) akikagua mifumo ya miundombinu mingine ya maji,umeme,gesi,tehama mawasiliano na zimamoto na uokoaji inayojengwa sambamba na ujenzi wa barabara inayojengwa mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.
Katibu wa kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Uratibu wa ujenzi wa mji wa Serikali Meshack Bandawe (mwenye koti la blu) akitoa maelekezo kwa mkandarasi wa ujenzi wa barabara za lami za mji wa Serikali China Heinan International Cooperation Co. Ltd (CHICO) wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo Mtumba jijini Dodoma.
Katibu wa kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Uratibu wa ujenzi wa mji wa Serikali Meshack Bandawe (wa kwanza kushoto) akipitia taarifa fupi ya ujenzi wa barabara za lami za mji wa Serikali alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo Mtumba jijini Dodoma.
********************************************
Ujenzi wa barabara za kiwango cha lami katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma wenye gharama ya bilioni 88.1 na urefu wa kilomita 51.2 umefikia asilimia 56.
Hayo yamesemwa na Katibu wa kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na Uratibu wa ujenzi wa mji wa Serikali, Meshack Bandawe wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo jijini Dodoma.
“Sasahivi kinachoendelea ni ujenzi wa barabara za lami zinazozunguka ndani ya mji wa Serikali na ujenzi huu umefikia sehemu nzuri na ikifika Julai mwaka huu utakuwa umekamilika”, aliongeza Bw.Bandawe
Aidha amesema ujenzi huo unahusisha ujenzi wa barabara za njia mbili za urefu wa kilomita 22.4 na zile zenye njia moja zenye urefu wa kilomita 28.8,pamoja na ujenzi wa miundombinu mingine kama maji, umeme,gesi,tehama mawasiliano,zimamoto na uokoaji,maduka makubwa pamoja na huduma za treni nk.
Katika hatua nyingine amesema ujenzi wa ofisi awamu ya pili utaanza baada ya kupata kibali hivi karibuni.
Mradi wa ujenzi wa barabara za mji wa serikali mtumba unatekelezwa na mkandarasi China heinan international cooperation co. Ltd (chico) na Unasimamiwa na wakala wa barabara za vijijini na mijini (Tarura), ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mwezi Machi 2019.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment