GCLA yatoa elimu ya vinasaba kwa wanasheria | Tarimo Blog

Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fedelice Mafumiko akizungumza wakati akifungua mafunzo ya vinasaba kwa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) Magdalena Mlolore akitoa maelezo kuhusiana na umuhimu mafunzo ya vinasaba kwa mawakili yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanasheria katika Mafunzo ya vinasaba.


*TLS waishukuru ofisi ya mkemia mkuu wa serikali 

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv.
MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA)  imesema kuwa mawakili ni muhimu sana kwao ni moja ya kundi omabaji wa matokeo ya vinasaba kwa ajili ya ushahidi.

Akizungumza katika Mafunzo ya Mawakili  yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkeamia wa Serikali, Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt.Fidelice Mafumiko amesema vinasaba vinatumika katika masuala mbalimbali ukiachana na kutafuta uzao kwa mama au baba dhidi ya kutafuta uhalali wa mtoto.

Dkt.Mafumiko  amesema GCLA itaendelea kushirikiana na  Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS)  katika utoaji wa huduma  na kusaidia shughuli za utoaji wa haki nchini.

Amesema kuwa lengo  la GCLA  kuwapatia elimu  wanasheria wa Chama Cha Wanasheria Tanzania (TLS) moja wawaze kujua kazi ya GCLA na majukumu ikiwa TLS ni  mdau muhimu katika utekelezaji wa baadhi ya majukumu ya GCLA ikiwemo utoaji wa huduma za uchunguzi wa vinasaba pale panapohitajika ushahidi mahakamani.

“Kwa mujibu wa sheria ya vinasaba vya  binadamu ya mwaka 2009 namba  8 kifungu  cha 26,mawakili wametajwa kama moja ya Taasisi  ombaji wenye jukumu kisheria la kuwasaidia wananchi kwa kuwaombea  na kupata huduma za uchunguzi wa vinasaba  na kukatua changamoto zinazowakabili kwa kutumia teknolojia ya vinasaba  vya binadamu”amesema.

Dk.Mafumiko alisema GCLA imeamua kutoa mafunzo hayo ili kuwajengea wanasheria uelewa juu ya teknolojia ya inasaba vya binadamu,taratibu za uchunguzi  wa vinasaba na kuelewa tafsiri ya matokeo pale panapohitajika.

“Mafunzo haya kwetu  yanafungua  ukurasa mpya wa TLS na GCLA katika utoaji wa huduma na kusaidia shughuli za utoaji wa haki nchini, GCLA itaendelea kushirikiana na wanasheria pamoja na kuendelea kuboresha huduma kwa weledi kama vioapo vinavyosema katika maadili  kupitia mabadiliko ya sheria  na kanuni mbali lmbali pale panapohitajika”amesema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TLS Maqdalena Mlolere amesema wanasheria 100 wamepatiwa mafunzo  kwa njia ya ana kwa ana huku zaidi ya 500 wakipatiwa kwanjia ya mtandao na kuongeza kuwa mwitikio kwa mawakili umekuwa mkubwa.

Amesema licha ya baadhi ya Mawakili wanaweza kuwa wanajua kazi za mkemia lakini baadhi yao wanaweza wakawa hawajui kutokana na uchanga wao hivyo mafunzo yamekuja kwa muda mwafaka.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2