WATANZANIA WATAKIWA KUTOKUWA NA HOFU BADALA YAKE WAMUOMBE MUNGU | Tarimo Blog

Na Woinde Shizza , Michuzi Tv-Arusha
WATANZANIA wametakiwa kutoogopa, kutoingiwa na hofu wala kuogopeshwa na magonjwa yanayokuja mara kwamara badala yake kila mmoja aombe kwa imani ili magonjwa haya yaondoke.

Aidha pia wametakiwa kumuweka Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli katika maombi ili aendelee kuwa na nguvu na msimamo wake wa kumuamini Mungu anaweza kutenda kila jambo.

Hayo yamebainishwa na askofu mkuu wa kanisa la intanational Evangelism,Dkt. Eliudi Isangya lililopo Katika Kijiji Cha Sakila kata ya Kikatiti wilayani Arumeru mkoani hapa ambapo alisema kuwa ni wajibu wa kila mtanzania kupiga magoti na kuomba kwa imani yake ili ugonjwa huu wa kushindwa kupumua (covid-19 )uweze kuondoka.

Alisema kuwa kufuatia agizo lililotolewa na Rais Magufuli la watanzania kufanya maombi ya siku tatu ya kuombea nchi juu ya janga hilo kanisa hilo limeungana na waumini wote nchini kuliombea taifa la Tanzania ili liondokane na magonjwa mbalimbali yanayoingia hapa nchini.

"Jambo hili linamgusa kila mtanzania, hivyo kila mmoja wetu aombe kwa nafasi yake Ili magonjwa haya mbalimbali yaweze kuondoka, niseme tu ata Yesu alijaribiwa na shetani akampeleka nyikani lakini pamoja na kujaribi wa Yesu alimshinda, lakini biblia inasema pamoja alishinda lakini shetani alimuacha kwa muda ila alimrudi tena, niseme na sisi mwaka jana 2020 shetani alitukaribu lakini tulimshinda akatuacha, akakapembeni akaona Kama tumesahau amerudi tena mwaka huu lakini naimani tutamshinda tena na tena kwakuwa sisi ni Wana wa Mungu na tumepewa mamlaka." Alisema Isangya

Aidha pia walitumia ibada hiyo kuomba maombi ya kuwafukuza nzige walioingia Wilayani Longido ambapo alisema kuwa wanahitaji mungu awaondoee kwani wataharibifu mazao na hivyo kufanya kuwepo kwa baa la njaa.

Kwa upande wa mmoja wa waumini hao Rogathe Mushi alisema kuwa kitu ambacho kinaweza kutusaidia ni kuomba kwa imani maana Mungu anasikiliza watu wenye imani, tukikenga imani hamna jambo ambalo litatushinda.

Alisema hakuna kitakacho tupata hapa Tanzania ,hamna ugonjwa wa Covid utakao tuiwa ,Wala nzige watakao kula mazao yetu maana watanzania tunaimani na Rais wetu pia anaimani.
Askofu mkuu wa kanisa la intanational Evangelism Tanzania Dr.Eliudi Isangya akiongoza waumini wanaoabudu Katika makao makuu ya kanisa hilo yaliopo sakila ,kata ya kikatiti wilayani arumeru maombi ya kuombea taifa kuondoka kwenye janga la ugonjwa wa Covid 19 pamoja na kuwafukuza nzige waliovamia katika mashamba yaliopo wilayani Longido (picha na Woinde Shizza , ARUSHA).

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2