WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTUMIA VYEMA KALAMU ZAO KUELEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI MBALIMBALI YA KIUCHUMI KATIKA UJENZI WA TAIFA. | Tarimo Blog

WAANDISHI wa habari wametakiwa kutumia vyema kalamu zao katika kueleza utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kiuchumi inayotekelezwa na kuchangia maendeleo ya taifa na hiyo ni pamoja na kueleza mipango ya kuelekea uchumi wa viwanda, changamoto na namna ya kuzitatua ili wananchi waweze kujua kinachofanywa na Serikali.

Akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa semina ya waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha katika tawi la Benki Kuu Mtwara kwa niaba ya Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT,) Bwa. Julian Banzi, Meneja wa Fedha na Utawala Mkoa wa Mtwara David Mponeja amesema, nafasi na uzito wa vyombo vya habari ni muhimu katika kueleza ni nini Serikali inafanya katika sekta mbalimbali katika kufikia uchumi wa viwanda.

"Tumieni kalamu na vyombo vyenu kueleza agenda muhimu katika ujenzi wa Taifa, Wananchi wanataka kujua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kiuchumi ambayo ikikamilika itachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya taifa letu na hiyo ni pamoja na mchango wa kila mmoja katika kuyafikia mafanikio hayo." Amesema.

Ameeleza kuwa, kwa kiwango kikubwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT,) inaridhika na jinsi vyombo vya habari vinavyotoa habari zinazohusu sekta ya fedha na uchumi huku changamoto mbalimbali ikiwemo uwezo wa kutafsiri na kuchambua kwa kina taarifa mbalimbali za uchumi zinazotolewa na Benki kuu na taasisi nyingine za fedha na uchumi zikiendelea kufanyiwa kazi mara kwa mara.

Aidha amesema, wamekuwa wakitoa mafunzo ya mara kwa mara ili kukuza uandishi wa habari za uchumi na fedha na kuziandika kwa usahihi, kujenga uwezo wa kutafsiri na kuchambua taarifa hizo na kudumisha uhusiano wa kikazi baina ya BoT na vyombo vya habari.

"Ni imani yangu kuwa kupitia semina tutajifunza zaidi, baadhi ya misamiati na dhana mbalimbali zinazotumika katika habari na taarifa za kifedha zitajadiliwa na kufafanuliwa ili zitakapotumika zitumike kwa namna ambayo zitaeleweka vyema." Amesema.

Vilevile amewataka kusimama katika nafasi zao kwa kuandika masuala yenye tija katika wakati huu ambao taifa lipo mbioni kuelekea uchumi wa viwanda ifikapo 2025.

"Katika semina hii pamoja na mada nyingine mtajifunza pia namna ya kutambua upatu haramu na yataendeshwa kwa ushirikiano wa BoT, Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji Tanzania (CMSA.) hii itawasaidia kuwaepusha wananchi na kuwaonya namna ya kujiepusha na upatu haramu kupitia kalamu zenu."Amesema.

Semina hiyo ni mwendelezo wa Semina ambazo Benki Kuu ya Tanzania imekuwa ikiandaa kwa wanahabari kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Taifa.

Meneja wa fedha na Utawala BoT Mkoa wa Mtwara David Mponeja akisoma hotuba kwa niaba ya Mgeni rasmi Naibu Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT),Bwa. Juliana Banzi wakati akifungua semina ya siku tano ya Waandishi wa Habari za Uchumi,Biashara na Fedha inayofanyika katika tawi la Benki Kuu mkoani Mtwara.
Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano (BoT),Vicky Msina akimkaribisha Mgeni rasmi Meneja wa Fedha na Utawala BoT Mkoa wa Mtwara Bw.David Mponeja (wa tatu kulia) kufungua semina ya waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha katika tawi la Benki Kuu Mtwara kwa niaba ya Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bwa. Julian Banza leo Mkoani humo.
Meneja Msaidizi Idara ya uchumi Benki Kuu,Tawi la Mtwara,Aristedes Mrema akiwasilisha mada kuhusu Mwenendo wa Uchumi wa Tanzania pamoja na Tanzania kuwa ndani ya uchumi wa Kati katika Semina ya waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha iliofanyika leo katika tawi la Benki Kuu Mtwara.Mkuu wa Maendeleo ya Uchumi BoT Bw.Mussa Mziya akiwasilisha Mada katika Semina ya waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha uliofanyika leo katika tawi la Benki Kuu Mtwara.













Mkuu wa Maendeleo ya Uchumi Tawi la Benki Kuu (BoT Mtwara Bw.Mussa Mziya akiwasilisha Mada katika Semina ya waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha uliofanyika leo katika tawi la Benki Kuu Mtwara.



Waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo inayohusu habari za uchumi, biashara na fedha katika ukumbi wa mkutano tawi la Benki Kuu Mtwara.
Mkuu wa Maendeleo ya Uchumi BOT Bw.Mussa Mziya akiwasilisha Mada katika Semina ya waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha uliofanyika leo katika tawi la Benki Kuu Mtwara.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2