Bolt Yaboresha Usalama wa Madereva kwa Mfumo wa Masaa 12 kwa Madereva | Tarimo Blog

 

Bolt, kampuni inayoongoza ya usafiri kwa njia ya mtandao nchini Tanzania, imezindua mfumo mpya unaoruhusu madereva kutumia mfumo huo kwa jumla ya masaa 12 pekee kwa siku. 

 

Mfumo huu unalenga kuhakikisha kuwa madereva wote wanafika kazini wakiwa wamechangamka na unalenga kupunguza ajali za barabarani zinazotokana na uchovu wa madereva. 

 

Mfumo huu wa masaa 12 pia utawapatia madereva muda wa kutosha wa kufanya mambo mengine muhimu kama vile kujumuika na familia na kujiendeleza kibiashara na kielimu. 

 

Meneja wa Bolt nchini, Remmy Eseka amesema, “Mfumo huu wa usalama barabarani ni sehemu ya juhudi zetu kuboresha huduma kwa faida za madereva na wasafiri ambao ni muhimu kwa biashara yetu. Kuboresha mazingira ya kimwili na kiakili kwa madereva na wasafiri ni muhimu ili kuhakikisha wote wanafika salama popote wanapokwenda. Ni imani yetu pia kuwa mfumo huu mpya utapunguza matukio barabarani na kuboresha mahusiano baina ya madereva na wasafiri.”

 

Madereva ambao watapokea wateja kupitia mtandao wa Bolt sasa wanaweza kufanya kazi kwa jumla ya masaa 12 pekee. Baada ya masaa 12, dereva atazuiwa kutumia mtandao huo na atalazimika kupumzika kwa muda uliowekwa kabla ya kuruhusiwa kurejea kutoa huduma. Mfumo huu wa masaa 12 unawajumuisha madereva wa magari, bajaji na boda boda. 

 

Utafiti unaopatikana Arrive Alive unaonesha kuwa duniani, asilimia 20% ya ajali zote za barabarani zinatokana na uchovu wa madereva. Barani Afrika, tatizo hili linaaminika kuwa kubwa zaidi ambapo ushahidi unaonesha asilimia 60% ya ajali zote barabarani zinatokana na uchovu wa madereva. Waendesha vyombo vya moto ambao hawajapata muda wa kutosha wa kupumzika wana changamoto za kiakili zinazowazuia kufanya kazi kwa ufasaha na umakini.

 

 

Dondoo chache za kuwasaidia madereva ambao wanahisi kukosa umakini barabarani ni: 

  • Ikiwa umechoka, ACHA KUENDESHA

  • Egesha chombo chako mahali salama

  • Usiegeshe chombo chako kwenye kona. Ikiwa upo kwenye barabara kuu, tafuta sehemu ambapo kuna barabara inayochepuka na utafute sehemu salama ya kuegesha chombo chako, au simama katika eneo linaloruhusiwa kupumzika.

  • Kunywa vikombe kadhaa vya kahawa chungu 

  • Pumzika au lala kwa angalau robo saa. 

 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2