BYABATO AWATETEA WAPIGA KURA WAKE KERO YA KUUNGANISHIWA MAJI. | Tarimo Blog


Na Abdullatif Yunus

Naibu Waziri wa Nishati na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Advocate Stephen Byabato amewasilisha Kilio cha Wapiga kura wa Jimbo la Bukoba Mjini kuhusu adha kubwa wanayokumbana nayo wakati wanapohitaji Kuunganisha Huduma ya Maji nyumbani kwao, ambapo hutakiwa Kulipia Shilingi laki moja na Nusu pesa ambayo ni gharama kubwa.

Naibu Waziri Byabato amewasilisha Kilio hicho kwa Naibu Waziri wa Maji Mhe. MaryPrisca ambaye yupo Ziarani Mkoani Kagera, wakati wa Mazungumzo yaliyofanyika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa Kagera, mapema Machi Mosi alipofika katika Ofisi hizo.

Mhe. Byabato ameomba Serikali kupitia Wizara ya Maji kutizama upya gharama hizo na ikibidi gharama zipunguzwe kwakuwa Jimbo la Bukoba Lina Maji ya Kutosha, na pengine gharama hizo zilipwe kidogo kidogo.

Akijibu ombi Hilo Naibu Waziri wa Maji MaryPrisca ameeleza kuwa changamoto hiyo kwa Sasa ipo Mikoa mingi Nchini na kwamba tayari ushauri na maombi hayo yamekwishaanza kufanyiwa kazi na Wananchi watarajie Huduma hiyo kuwafikia nyumbani.

Kwa upande mwingine Naibu MaryPrisca amewashukuru Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) kwa namna ambavyo wameendelea kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maji Jimboni humo, na kuongeza kuwa amefurahishwa na kauli Mbiu yao Mpya ya Maji inayosema MAJI BOMBANI,BOMBA LIPI , BOMBA LA NYUMBANI na kwamba anaichukua itumike Nchi nzima
















Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2