Naam huyu ndiye Othman Masoud Othman, ambae alifutes kazi na mteule wake, rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein, na kumteua aliyekuwa naibu mwanasheria mkuu, Said Hassan Said, kuchukua nafasi yake.
Kwa mujibu wa taarifa ya serikali,iliyopatikana Oktoba 7, 2014 kwa vyombo vya habari Masoud amefutwa kazi kwa mujibu wa vifungu namba 53 na 54 (1) na 55 (3) vya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, na kifungu namba 12 (3) sheria ya utumishi wa umma ya Zanzibar ya mwaka 2011.
Itakumbukwa ya kwamba, Masoud, alijiondoa kwenye kamati ya uandishi ya bunge maalum la Katiba, bila ya kutoa sababu zozote huku akiwa mshauri mkluu wa sharia wa serikali hiyo na alionekana siku ya pili ya upigaji kura kuamua hatma ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayopendekezwa na bunge hilo.
Jambo lililowashtua wengi, katika kura yake ambayo ilikuwa ya wazi, alipiga kura ya hapana akikataa vifungu kadhaa vya katiba hiyo, hali iliyoamsha hamasa kutoka kwa baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kutoka Zanzibar, na kupiga makelele ya kutaka aondolewe kwenye nafasi hiyo.Hali hiyo iliwalazimu maafisa wa usalama wa bunge hilo, kumpatia ulinzi maal;um wakati akiondoka bungeni hapo ili kumuepiusha na kipigo kiutoka kwa wajumbe wa Bunge hilo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment