NAIBU WAZIRI WA MAJI ARIDHISHWA NA KASI YA RUWASA, AAHIDI KUPELEKA MAJI MUBABA SEKONDARI. | Tarimo Blog


Na Abdullatif Yunus.

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Mery Prisca Mahundi ameagiza kuharakishwa mchakato wa kupeleka maji katika shule ya Sekondari Mubaba iliyopo Wilayani Biharamulo ili kuondoa kero ya maji kwa wanafunzi na kuahidi kuifanyia kazi haraka ili kuitatua.

Naibu Waziri MaryPrisca ambaye yupo Mkoani Kagera katika ziara ya Kikazi amefika Shuleni na Kusikiliza kilio hicho cha Uhaba wa Maji, na kuelezwa kuwa kwa Kipindi Cha kiangazi ambapo, Wanafunzi hao wamekuwa wakilazikika kukatisha masomo yao kutembea mwendo mrefu muda wa Masomo kufuata maji Vijiji vya Jirani.

Akiwa katika mradi wa. Maji wa Kabindi, Naibu Waziri waipongeza wakala wa Maji Vijijini RUWASA Mkoani Kagera kwa Kasi waliyonayo katika kuhakikisha wanaondoka adha ya maji hasa kwa wilaya ya Biharamulo.

Ameongeza kuwa kutokana na jitihada ambazo RUWASA Wilaya ya Biharamulo walizonazo, Wizara itawaletea fedha kwaajili ya kupanua mtandao wa maji na kuanzisha miradi mipya kwenye maeneo ambayo bado Kuna kero ya maji.

"Niwapongeze Wananchi kwa kumchagua Mhe. Ezra Chiwelesa kuwa mbunge wenu, amekuwa akinisumbua kuhusu suala la maji na hapa nimekuja kufatilia maswali yake ya kutaka kumaliza kero ya maji Biharamulo,"

"RUWASA mnafanya vizuri niwapongeze Sana na kwa namna mnavyokwenda pesa tutaleta ili miradi mingi mliyonayo muweze kuimalizia."

Akiwa katika shule ya Sekondari Mubaba Naibu Waziri ameeleza kuanza mchakato wa kitaalamu ili kuweza kusogeza huduma ya maji shuleni hapo ambayo imekuwa changamoto ya muda mrefu na kupelekea wanafunzi kuhangaika.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi Mhe. Mhandisi Ezra Chiwelesa, amesema kuwa wilaya hiyo imekuwa ikitengewa bajeti finyu na kupelekea Maeneo mengi kutopata huduma ya maji.

Mhe. Ezra ameongeza kuwa licha ya shule ya Sekondari Mubaba kuwa na changamoto ya umeme, changamoto mama ni maji ambayo imekuwa ikiwapelekea wanafunzi hao kutembea umbali mrefu na muda mwingine kukosa masomo.

Wakizungumza kwa Nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa kata ya Kabindi wilayani Biharamulo mkoani Kagera wamesema katika kipindi ambacho miradi ya maji ilikuwa haijakarabatiwa walikuwa wanalazimika kunywa maji yasiyo safi na salama kutokana na kukosekana kwa maji ya bomba katika eneo hilo.

Hali hiyo imemsukuma Naibu Waziri wa maji MaryPrisca Mahundi kufika katika kata hiyo na kuzindua mradi wa maji uliogharimu kiasi cha shilingi milioni mia tatu ishirini na tano utakaoweza kuwahudumia vijiji vinne vyenye zaidi ya wananchi elfu kumi na nane(18,000).

 

………………………………………………………………………………………….

 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2