***************************************
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mwita Waitara, amefanya ziara katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa kutembelea Ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Manispaa ya Kinondoni na Manispaa ya Ubungo kujionea utunzaji na usimamizi wa mazingira katika maeneo hayo pamoja na changamoto mbalimbali za kimazingira.
Akiwa ofisi za Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) ameongea na Menejimenti ya Ofisi hiyo na kuwasisitiza kuendelea kusimamia hifadhi na utunzaji wa mazingira pamoja na hayo amewapongeza kwa kufanya kazi nzuri katika masuala yote yanayohusu mazingira. Akiongea katika kikao hiko Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nemc Dkt. Menan Jangu amemshukuru Naibu Waziri kwa kufika katika Ofisi za NEMC na kumuahidi kufanyia kazi maelekezo yake.
Akiwa Manispaa ya Kinondoni alitembelea eneo la Mwagwepande ambapo Manispaa hiyo wanajenga kiwanda cha kuchakata taka zitokanazo na mbogamboga na matunda na kupata samadi, pia ametoa maelekezo kwa Manispaa hiyo kusimamia vyema shughuli za uhifadhi na utunzaji wa mazingira. “Nawapongeza sana Manispaa ya Kinondoni kwa mradi huu mkubwa wa kuchakata taka naagiza Manispaa nyingine pia ziige mfano huu wa Manispaa ya Kinondoni” alisema Naibu Waziri Waitara.
Aidha alitembelea Manispaa ya Ubungo na kuongea na Menejimenti ya Manispaa hiyo na kupata taarifa ya mazingira katika Wilaya hiyo, akiwa katika Manispaa ya Ubungo alitembelea machinjio yaliopo katika Kata ya Kimara na kukagua utunzaji wa mazingira na mfumo wa majitaka ya machinjio hayo. Vilevile alitembelea Kiwanda cha Heghj Invenstment Ltd kilichopo katika Manispaa ya Ubungo na kujionea uendeshaji wa kiwanda hiko katika suala zima la utunzaji na uhifadhi wa mazingira. Mwisho aliwaagiza wataalamu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira kufanyia utafiti moshi unaotoka katika kiwanda hicho kujua kama una madhara au la.
Naibu Waziri Mwita Waitara yuko katika ziara ya siku tano katika Mkoa wa Dar es salaam akikagua masuala mbalimbali yanayohusu utunzaji na hifadhi ya mazingira katika mkoa huo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment