RITA YAWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI MKAKATI WA USAJILI MATUKIO KITAIFA | Tarimo Blog


Kaimu Kabidhi Wasii Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA,) Bi. Emmy Hudson (kushoto,) akiwasilisha taarifa kwa kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa Usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu Tanzania bara leo jijini Dodoma.




Uwasilishaji ukiendelea.


Wajumbe wa kamati wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa hiyo.
 


KAIMU Kabidhi Wasii Mkuu wa Wakala wa Usajili , Ufilisi na Udhamini (RITA,) Bi.Emmy Hudson hii leo Jijini Dodoma amewasilisha taarifa kwa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu Tanzania Bara.

Mkakati huo umelenga kuangalia masuala ya Mfumo wa Usajili, kupitia Sheria ya Usajili, kuboresha Mfumo wa TEHAMA na kuimarisha mahusiano baina ya Taasisi zinazohusika na majukumu ya usajili.

"Huu Mkakati ni wa Kitaifa na  unajibu matakwa na kuboresha hali ya Usajili wa Vizazi na Vifo na upatikanaji wa uhakika wa takwimu za matukio muhimu ya binadamu na kuwezesha Serikali kuimarisha mifumo yake ya maendeleo katika nyanja za uchumi, jamii,Siasa, ulinzi na usalama." Alisema Bi.Hudson.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2