Na Denis Mlowe Iringa
WANANCHI mkoani Iringa wametakiwa kufanya mazoezi ya viungo na kushiriki michezo mbalimbali ili kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanayosababishwa na mfumo wa maisha usiozingatia lishe bora.
Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa mgahawa wa kisasa wa Sweet Treats, ulioko mjini Iringa, Meddy Nahdi wakati wa bonanza la mazoezi liloshirikisha timu nane katika viwanja wa Garden vilivyoko manispaa ya Iringa.
Nahdi ambaye amejenga viwanja vya kisasa vya mchezo wa soka wa watu sita na mpira wa kikapu katika bustani ya Manispaa alisema kuwa wananchi wawe na tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza pamoja na yale yasiyo ya kuambukizwa ikiwemo virus vya corona.
Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa na mazoea ya kukaa bila kufanya mazoezi jambo ambalo linawasababishia kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara ikiwemo ya Moyo kutokana kutozingatia mazoezi .
"Mazoezi yanasaidia sana kuondoa magonjwa yasiyoambukiza kama sukari na presha ,pia huondoa usongo wa mawazo pamoja na kuleta mahusiano baina ya kundi na kundi ,mtu na mtu au na jamii nzima na muunganiko wa kazi kupitia mazoezi hayo",alisema
Alisema magonjwa hayo hutokana na kutokufanya mazoezi, kuwa na uzito wa juu na kula vyakula visivyozingatia lishe bora.
Aidha mbali na kufanya mazoezi alitoa wito kwa timu mbalimbali za veterans kutumia viwanja hivyo kwa ajili ya mazoezi kwa gharama nafuu kwani vimezingatia ubora wa viwango katika ujenzi wake.
Alivitaja vyanzo vingine vya magonjwa hayo kuwa ni uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe uliokithiri hivyo endapo watajenga tabia ya kufanya mazoezi itasababisha waondokane na kutumia hivyo vitu.
“Kwa bahati mbaya, magonjwa haya hayana dalili katika hatua za mwanzoni lakini dalili huanza kuonekana pale madhara sugu yanapoanza kuonekana. Magonjwa haya ni kisukari, shinikizo la damu na saratani” alisema
Kwa upande wake mkurugenzi wa Masari Investment, Faraj Abri ambao wanajishughulisha na uuzaji wa rangi mbalimbali za nyumbani na magari alisema kuwa mazoezi ni jambo la msingi katika kuhakikisha jamii inaepuka magonjwa hayo.
Aliwomba wananchi kujitokeza kwa wingi katika bustani ya Manispaa kufanya mazoezi ambapo Kuna viwanja vya kisasa vya michezo.
Alisema kuwa kitendo cha wananchi kuwa na mazoea ya kufanya mazoezi ni sawa na chakula ubongo kwani ni muhimu na husaidia sana kuwa afya niema ili waweze kuchapa kazi na kuivusha Tanzania kwenda nchi ya uchumi wa kati.
Viwanja vya kisasa vya vilivyoko katika bustani ya Manispaa ya Iringa ambavyo wengi wamekuwa wakitumia kwa ajili ya mazoezi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment