*Wadai walimu wanalazimishwa kujiunga na CWT
*Maafisa Utumishi na Wakurungenzi wawa sehemu ya madalali wa kuwachagulia vyama
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
CHAMA cha Kutetea na Kulinda Haki za Walimu Tanzania (Chakuhawata) kimesema hakiridhishwi mwenendo wa kukatwa walimu katika vyama viwili.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa malalamiko ya walimu kwa muda mrefu kuhusiana na makato yanayofanywa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na kuamua kuanzisha vyama vingine vyenye maono ya kuwakomboa walimu.
Wakizungumza na Mwandishi wa Habari hizi Mwalimu Emmanuel Patrick amesema kuwa hakuna sababu ya kukatwa vyama viwili wakati mtu anaingia kwenye Chama cha Taaluma kutokana na matakwa yake.
Mwalimu Patrick amesema kuwa tararibu za utumishi zinaruhusu mtumishi kujiunga kwenye Chama anachotaka lakini kwa upande walimu wanalazimishwa kujiunga na CWT bila ridhaa huku makato yakifanyika kwa vyam viwili na kufanya maisha kuwa magumu.
Aidha Chakuhawata kinakata Mwanachama sh.5000 ambazo kazi yake zinafanya na kumfanya Mwalimu kuwa sehemu salama.
Naye Mwalimu wa Noor Bankineza amesema kuwa maisha yamekuwa magumu kutokana na CWT wanakata asilimia 2 ya mshahara ambao ni kubwa katika kufanya makato hayo.
Amesema kuwa kuwa walimu walioko CWT wameshinikizwa na maafisa watumishi pamoja na wakurungenzi huku fitina zikiwa kubwa za kutaka kuu Chakuhawata.
Mwalimu Agustino Jackson ambaye ni Katibu wa Chakuhawata Manispaa ya Temeke amesema kuwa licha ya kuwepo kwa malalamiko wanaiomba serikali kuangalia malimbikizo ya fedha za likizo tangu mwaka 2016.
Jackson amesema kuwa vyama vya wafanyakazi vifanye kazi yao wanachama isitokee wakaibuka Miungu watu wa kuaminisha Chama kilichopo ni CWT.
Aidha amesema kuwa wamekuwa wakikatwa na CWT lakini hakuna faida yeyote hata kushindwa kutengeneza Tisheti kwa ajili ya Siku ya Wafanyakazi ambayo hufanyika Mei Mosi ya kila mwaka.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment