Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Theodosia Muhulo (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam leo Aprili 30, 2021. Wakwanza kushoto ni Katibu wa wafanyakazi SBS, Crement Bundi, Kutoka Kulia ni Sekela Kanamela na wapili kulia ni Mwalimu Bhoke Makulu.
Katibu wa wafanyakazi SBS, Crement Bundi akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam leo.
Sekela Kanamela wa kwanza kulia akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam leo.
KUELEKEA siku ya wafanyakazi Mei Mosi, 2021 kituo cha Msaada wa Sheria kwa wanawake (WLAC) wametoa wito kwa waajiri, Serikali na wadau mbalimbali kuweka mifumo wezeshi na mazingira mazuri ya ajira ikiwemo kuweka sera na kufanya mabadiliko ya kisheria zenye kuzingatia usawa wa kijinsia.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam leo Aprili 30, 2021 Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Theodosia Muhulo amesema kuwa WLAC kupitia Mradi wa uwezeshaji wa jamii kisheria juu ya sheria na haki za ajira wamefanikiwa kutoa elimu kwa wanawake zaidi ya milioni nne.
Theodosia amesema kuwa kupitia Mradi huo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wameweza kujitokeza kituo cha Msaada wa Sheria kwa wanawake (WLAC) kudai haki zao.
Hata hivyo Theodosia ametoa wito kwa wanawake kujitambua na kuwa na ujasiri wa kupambani haki zao pale wanapoona haki zao zinayumbishwa.
Licha ya hayo matokeo yaliyojitokeza katika Mradi unaofadhiliwa na Shirika la Legal Serivices Facility waajiriwa wengi wameelimika baada ya kuelimishwa na wamefanikiwa kufuata sheria na taratibu za ajira.
Amesema kuwa waajiri nao wameweza kuwapa mikataba ya ajirà , likizo na kuzingatia makato yaliyoainishwa kisheria wafanyakazi wao
Katika kipindi cha Utekelezaji wa Mradi huo WLAC, imewafikia wafanyakazi 672 ambao kati yao wanawake ni 432 ambao wameweza kupata msaada wa kisheria katika mashauri yao.
Naye katibu wa chama cha wafanyakazi SBC, Bundi Clement, amesema WLAC imekuwa mkombozi mkubwa katika kutoa elimu na ushauri kwa wafanyakazi ambapo wengi wao wameweza kufaidika na kufurahia.
Kumekuwa na elimu ya kutosha kutoka WLAC uliopelekea wafanyakazi kutambua hazi zao kazini na pia elimu yao imepunguza migogoro mbali mbali ambapo awali kabla hatujapata elimu ya kazi basi ilikuwa hata jambo dogo linaleta usumbufu na kulifanya kubwa lakini sasa tumekuwa washauri wa mwajiri.
Kwa upande wake, Bhoke Makulu ambaye ni Mwalimu, ameishukuru WLAC kwa kusaidia wanawake wanaonyanyasika kazini.
Amesema yeye alikuwa akifundisha shule binafsi lakini mkataba wake ulikatishwa bila kufuata utaratibu lakini WLAC walimsikiliza.
"Kwa kweli, hapa ni mahali ambapo nilikuwa na uwezo wa kujieleza na kusikilizwa bila kukatishwa tamaa, ninatoa wito kwa kwa wanawake wote mnaokutana na changamoto kazini na hata unyanyasaji wa namna zote kufika WLAC kupata msaada." Amesema
Naye katibu wa chama cha wafanyakazi SBC, Bundi Clement, amesema WLAC imekuwa mkombozi mkubwa kwa wafanyakazi katika kutoa elimu na ushauri kwa wafanyakazi ambapo wengi wao wameweza kufaidika na kufurahia.
Kumekuwa na elimu ya kutosha kutoka WLAC uliopelekea wafanyakazi kutambua haki zao kazini na pia elimu yao imepunguza migogoro mbali mbali ambapo awali kabla hatujapata elimu ya kazi basi ilikuwa hata jambo dogo linaleta usumbufu na kulifanya kubwa lakini sasa tumekuwa washauri wa mwajiri.
"Kadri WLAC inavyozidi kuwasiliana nasi na kutoa elimu ndivyo na sisi tunavyopata nafasi ya kutenda haki kwa wale tunaowaongoza." Amesema Bundi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment