Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amependekeza jina la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo kuwa Katibu Mkuu wa Chama Mapinduzi na kushina nafasi ya aliyekuwa katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Bashiru Ally.
Hayo yametokea leo Mkoani Dodoma leo Aprili 30, 2021 mara baada Mwenyekiti wa CCM Rais Samia kushika kijiti cha aliyekuwa Mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Hata hivyo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Chritina Mdeme ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment