Vijana wa Kujitolea JKT Warejeshwa Katika Mafunzo | Tarimo Blog

Na Mwandishi wetu- Dodoma

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Charles Mbuge, amewarejesha katika mafunzo vijana waliochaguliwa kujiunga na  JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2020/2021 baada ya kurejeshwa nyumbani mwezi Februari 2021.

Akitoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari, Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala  JKT Kanali Hassan Mabena  amesema, vijana hao wanatakiwa kuripoti  katika kambi  walizokuwa wamepangiwa awali kuanzia Mei 7 hadi 14. Amefafanua kwamba vijana waliorejeshwa ni wale wenye elimu ya Darasa la Saba na Kidato cha Nne.

“Vijana wenye Elimu ya Kidato cha Sita, Ngazi ya Cheti, Stashahada, Shahada na wale wenye Taaluma ya Uhandisi wataendelea kusubiri majumbani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa,” alisisitiza Kanali Mabena.

Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT) limekuwa likiendesha mafunzo yakuwajengea uwezo vijana kwa kuwapa stadi za maisha ikiwa ni pamoja na uzalishaji mali, uzalendo, kilimo, ufugaji na kushiriki katika ujenzi wa Taifa.

Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kanali Hassan   Mabena akitoa taarifa ya kurejeshwa kwa  vijana wa kujitolea katika mafunzo ya JKT kuanzia Mei 7 hadi 14, 2021 baada ya kuwarejesha nyumbani hapo awali.

 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2