Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma leo Aprili 13, 2021 Rais wa Chama cha Walimu Tanzania Mwalimu Leah Ulaya amesema majukumu yaliyooneshwa kwenye bodi hiyo yanafanana na yale yanayofanywa na Tume ya Utumishi wa walimu [TSC] iliyopo sasa.
“Mnamo mwaka 2019 , Chama cha walimu Tanzania kilialikwa kutoa maoni kuhusu uanzishwaji wa Bodi hiyo kimsingi sisi CWT,tuliikataa kwa nguvu zote baada ya kusoma sheria hiyo tukajiridhisha pasi na shaka kwamba chombo hiki kililenga kumgandamiza mwalimu badala ya kumsaidia ,aidha majukumu yaliyo kwenye bodi hiyo yanafanana na yale yanayofanywa na Tume ya utumishi wa walimu.'' Amesema Ulaya
Rais huyo wa CWT ameendelea kufafanua kuwa;
”Mnamo Tarehe 12 April,2021 CWT tulialikwa na katibu wa bunge kukutana na kamati ndogo ya Bunge ya sheria juu ya kanuni za uendeshaji wa bodi hiyo ambayo msingi wake ni sheria mama ambayo sisi CWT tulikataa tangu mwanzo,katika kikao hicho cha tarehe 12,April,2021 Chama cha Walimu Tanzania kiliendelea na msimamo wake wa usitishwaji wa chombo hiki na kuimarisha utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu[TSC.]
Aidha, Rais huyo wa CWT ametaja sababu kadhaa za msimamo kupinga uwepo wa bodi hiyo kuwa ni pamoja na gharama za bodi ambapo uendeshwaji utategemea pesa ya mwalimu mfukoni na ada ni elfu hamsini kwa mwaka pamoja na kupunguza utitiri wa vyombo vinavyomsimamia mwalimu.
“Bodi hii tunaipinga kwa nguvu zote kwa sababu ,uendeshaji wa bodi hii utategemea pesa ya walimu mfukoni kwa ajili ya usajili,leseni na ada kwa mwaka ambayo si chini ya Tsh.50,000/=,gharama za kusikiliza mashauri,gharama za semina ya kila mwaka ambayo ni lazima kuhuisha leseni hiyo ,kushindwa kufanya hivyo mwalimu atanyang’anywa leseni na hivyo kupoteza sifa ya kufundisha na sababu nyinyine ya kuikataa bodi hii ni kupunguza utitiri wa vyombo vinavyomsimamia mwalimu na majukumu yakifanana.” Amesema.
Makamu wa Rais wa CWT Dinah Mathamani ameiomba serikali kuendelea kuwamini na kuwatia moyo walimu.
“Walimu tunafanya kazi kwa bidii na ukiangalia ufaulu umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka kinachotakiwa ni serikali kuendelea kuamini walimu pamoja na kuwatia moyo.'' Amesema.
Katibu mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania[CWT] Deus Seif amesema endapo bodi hiyo itapitishwa makato ya mwalimu kila mwezi itakuwa ni Tsh. 4200 huku Naibu katibu Mkuu CWT,Maganga Japhet Bodi ya kitaaluma ya Walimu Tanzania haina faida yoyote bali itadidimiza uchumi wa walimu.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment