Mkurugenzi TAMWA ataka jamii isiwashangae wanawake kuwa viongozi | Tarimo Blog

Wanahabari tofauti kutoka Tanzania wakibadika karatasi ambazo zinalenga kuonesha ni vitu gani wanapaswa kufanya wanaume na vitu gani ambavyo vinapaswa kufanya wanawake na ni vipi wanaweza kufanya wote kwa pamoja.
Mwandishi wa habari kutoka gazeti la Daily news kwa upande wa Zanzibar Issa Yussuf akichangia miongoni mwa mada zilizowasilishwa katika mafunzo hayo.
Mwakilishi wa shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa.UNESCO Nacy Kaizilege akitoa neon kwa niaba ya shirika hilo.
Mkurugenzi wa TAMWA Rose Reuben akifungua mafunzo ya siku tatu kwa waandishi wa habari 30 Tanzania yenye lengo la kuwawezesha wanahabari hao kuandika habari za kijinsia pamoja na umuhimu wa uongozi kwa wanawake.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo tofauto wakijianda kubadika karasai ambazo zinalenga kuonesha ni mambo gani anayostahiki kufanya mwaname na mwanamke.

Na Muhammed Khamis, TAMWA
MKURUGENZI wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Rose Reuben amesema wakati umefika kwa jamii kubadili mtanzamo na kuona kuwa nafasi ya uongozi kwa mwanamke sio bahati bali ni jambo analostahiki kama walivyo wanaume.

Aliyasema hayo katika ukumbi wa White Sand hote Mbezi Jijini Dar Es Salam katika mafunzo maalumu ya siku tatu ya waandishi wa habari 30 kutoka vyombo tofauti Tanzania yaliolenga kuwajenga uwezo waandishi hao kuhusu maswala ya kijinsia na umuhimu wa uongozi kwa wanawake.

Alisema wanawake katika jamii bado wanaonekana si watu wenye kustahiki kuwa viongozi na ndio maana uwepo wa Rais Samia madarakati hadi leo hii kuna watu wanaendelea na mshangao.
Kufuatia dhana hiyo Mkurugenzi huyo alisema waandishi wa habari ndio wenye wajibu wa kubadili mitazamo hio kwa jamii ili waweze kuamini kuwa mwanamke ni kama sehemu nyengine ya wanaopaswa kuwa viongozi.

Alisema kwa kuwa wanahabari wana sauti kubwa kuliko watu wengine ama taasisi basi wanapaswa kutumia vyema fursa walionayo kuibadili jamii ya kitanzania kutoka kwenye mawazo yasiopaswa kuwepo hadi sasa.

‘’Tunahitaji kuona mifumo ya usawa kwenye jamii zetu ili wanawake wasiedelee kuonekana kuwa watu dhaifu na wasiofaa kushika nafasi mbali mbali za uongozi.’’Aliongezea.

Kwa upande wake mwakilishi wa Shirika la umoja wa kimataifa linalojihusisha na maswala ya wanawake UNWOME Hodan Addov alisema wataendelea kushirikia na TAMWA katika pande zote mbili kwa lengo kwa lengo la kuleta usawa katika jamii.

Alieleza kuwa anaamini uwepo wa usana ni dhana inayostahiki kuwepo kwa lengo la kujenga Tanzania imara kwa watu waote bila upande mmoja wa jinsia kuonekana kuwa na nguvu zaidi na mwengine ni dhaifu.

Nae mwakilishi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa.UNESCO Nacy Kaizilege alisema wanahabari wanawajibu kupasa sauti zaidi za wanawake kupitia taarifa zao za kila siku huku wakijua kuwa wanawake ni watu wanaohitaji kupaziwa sauti zao zaidi.

Sambamba na hilo aliwataka pia wanahabari hao kutoacha kupaza sauti zao kuhusu maswala ya udhalilishaji katika Nyanja mbali mbali zikiwemo za kisiasa ambapo hadi sasa kumekuwepo na taarifa mbali mbali za udhalilishaji kwa wanawake kupitia siasa.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2