KIMBUNGA JOBO KULETA ONGEZEKO LA UPEPO NA MAWIMBI BAHARI YA HINDI | Tarimo Blog


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema kumejitokeza mgandamizo mdogo wa hewa ambao umefikia kiwango cha kimbunga hafifu kwa jina Jobo kaskazini mwa kisiwa cha Madagascar.

Uwepo wa kimbunga hicho unatarajiwa kusababisha ongezeko la upepo na mawimbi katika bahari ya Hindi hususan katika Pwani ya mwambao wa mikoa ya Mtwara na Lindi. 

Katika taarifa iliyotolewa na TMA leo Aprili 21, 2021 imesema, Kimbunga hicho kipo kaskazini mwa Kisiwa cha Madagascar katika Bahari ya Hindi umbali wa Kilometa 930 na kilometa 1030 kutoka pwani ya Lindi na Mtwara. 

Aidha Mamlaka imesema inaendelea kufuatiliia mwenendo na mwelekeo wa kimbunga Jobo kwa kuzingatia mifumo mingine ya hali ya hewa iliyo jirani zaidi na kimbunga hicho ambayo inaweza kubadili nguvu na mwelekeo wa kimbunga Jobo katika wakati ujao.

Wananchi wametakiwa kuendele kuzingatia tahadhari ya upepo na mawimbi iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania katika maeneo husika itaendelea kutoa taarifa kila inapobidi.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2