Mbali na wanandoa hao mshtakiwa mwingine ni Nourdine Youssouf (43) Mkazi wa Kariakoo.
Pia mahakama imeamuru kutaifishwa EURO 6450 walizokamatwa nazo washtakiwa hao kuwa mali ya serikali na ameamuru mihuri hiyo iharibiwe chini ya uangalizi wa serikali.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Kassian Matembele amesema ametoa adhabu hiyo kwa washtakiwa kwa kuzingatia shufaa za washtakiwa na kwamba wamekaa gerezani muda mlefu na kwamba ni wakosaji wa mara ya kwanza.
Hata hivyo, washtakiwa hao tayari wameshailipa serikali fidia ya Sh milioni 15 kama walivyoingia makubaliano na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP.)
Mapema, wakili wa serikali Faraji Nguka akiwasomea hoja za awali washtakiwa hao pamoja na mambo mengine amedai, Septemba 5 mwaka 2019 eneo la Kariakoo Mtaa wa Kongo, mshtakiwa Nourdine na Nadhifa walikamatwa na polisi ambapo baada ya kupekuliwa katika makazi yao, walikamatwa na hati zao za kusafiria ikiwemo ya Twahili Raia wa Comoro Mkazi wa Magomeni Kisiwani ambaye ilibainika ni mume wa Nadhifa.
Imedaiwa, polisi na washtakiwa hao ,walienda kwa Twahili na alipopekuliwa walikutwa na hati za kusafiria, shaba za Kitanzania, mihuri 35 ikijumuisha ya idara ya Uhamiaji Tanzania, Comoro, Zambia, Uganda na ya serikali ya mtaa Temeke, kinondoni na Ilala.
Vingine ni vyeti vya ndoa, stika za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TPA) na walipohojiwa katika kituo cha polisi kati washtakiwa hao walikiri kujihusisha na biashara haramu ya kusafirisha binadamu.
Ilidaiwa kwamba, washtakiwa hao walikutwa na hati hizo za kusafiria ili ziwasaidie kwenda Italia na Ufaransa wakitoka Tanzania ambapo kila safari iliwagharimu kati ya Euro 300 hadi 640.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment