Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako(kulia) akimkabidhi cheti Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo baada ya kuhitimu Programu za Uongozi kutoka Uongozi Istitute.Katikati ni Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Deogratius Ndejembi
Sehemu ya wahitimu wa programu za Uongozi waliohitimu katika Taasisi ya Uongozi wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na viongozi waliohudhuria mahafali hayo yaliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako aliyemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.Sehemu ya wahitimu wa mafunzo ya programu za uongozi wakiwa kwenye mahafali hayo.
Mhitimu wa Cheti cha Uongozi kutoka Taasisi ya Uongozi Institute Turphina Matekere akiwa na wahitimu wengine wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye mahafali hayo.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
WAHITIMU wa mafunzo ya programu za uongozi waliohitimu katika Taasisi ya Uongozi Institute ambao wengi wao ni viongozi katika taasisi za umma na sekta binafsi wametakiwa kuyatumia mafunzo waliyoyapata kuleta chachu ya utendaji na uongozi bora sehemu za kazi.
Wametakiwa kuhakikisha wanakuwa viongozi ambao wanakwenda kuleta umoja badala ya mifarakano katika taasisi wanazoziongoza huku wakishauriwa kuyatumia mafunzo hayo kutatua na kumaliza migogoro sehemu za kazi.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wakati wa mahafali ya nne ya Taasisi ya Uongozi Institute yaliyofanyika Mlimali City jijini Dar es Salaam.Waziri Ndalichako alimwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi.
"Wakati mnaanza mafunzo haya naamini mlikuwa na jambo fulani hivi mnataka kulifikia kwani kuna wengine walishakuwa viongozi lakini wameamua kuka kupata mafunzo ya uongozi,mlikuwa mnataka kujengewa uwezo zaidi ya mliokuwa nao na mnataka kuhakikisha maeneo ambayo mnayasimamia yanakuwa bora zaidi.
"Huu ni muafaka wa kujitazama tena kabla ya mafunzo haya na baada ya mafunzo ili kuona mmebadilika kwa kiasia gani na kisha kwenda kubadilisha wengine, kuhitimu kwenu kunaashiria mmepikwa na mmeiva na mtakuwa mfano bora katika vituo vyenu vya kazi.
"Mkawe washauri na wasimamizi wazuri katika maeneo yenu mnayosimamia, naamini Serikali na taasisi mnaziongeza zimewekeza kwenu zikiamini uwekezaji huu unakwenda kulipa kwani umekwenda sehemu sahihi, miongoni mwa sifa za viongozi bora ni kuongea mshikamano kazini ili kuleta tija,"amesema Profesa Ndalichako.
Amefafanua migogoro kazini haina tija, haina afya pahala pa kazi na kiongozi bora hawezi kuruhusu migogoro kazini ingawa kuna baadhi ya maeneo mengine viongozi ndio wanachochea migogoro kazini, kupitia wahitimu hao hawatarajii kuona wakiwa chanzo cha migogoro bali kuwa chachu ya kuonesha uongozi uliobora.
"Naaamini wahitimu hawa watakuja na mbinu mpya za uongozi na kuleta matokeo chanya, tunafahamu nchi yetu iko kwenye mpito baada ya kufariki dunia kwa aliyekuwa Rais wa Serikali wa Awamu ya Tano chini ya Hayati Dk.John Magufuli, na sasa tunaye mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan, tuna kila sababu ya kuhakikisha sote tunampa ushirikiano.
"Mliohitimu leo wengi wenu ni viongozi katika taasisi mnazotoka , kupitia mafunzo haya mtakuwa na kitu cha ziada kuhakikisha shughuli za Serikali ya Awamu ya Sita shughuli za kuleta maendeleo zinaendelea chini ya Rais wetu mpendwa Samia Suluhu Hassan,"amesema.
Awali mmoja ya wahitimu wa mafunzo hayo ya uongozi katika taasisi hiyo, Saada Mkuya Salum amesema kitoa salamu za wahitimu hao, amesema wanatoa shukrani kwa Uongozi Institute kwa kuratibu mafunzo hayo kwao na kuhakikisha mafunzo hayo yanakuwa yenye tija kwa wahitimu wote.
"Katika kipindi chote ambacho tulikuwa tunapatiwa mafunzo haya , tunakumbuka tulikumbana na changamoto ya janga la Corona lakini Uongozi Istitute waliamua kuangalia namna ya kuhakikisha tunaendelea kusoma, tunashukuru kwa jitihada zao.Sisi ni viogozi lakini uonozi ni kuhakikisha unaleta mabadiliko kwa wale tunawaongoza, tumepikwa, tumeiva.
"Tumepata mafunzo yanayohusu uongozi katika nyana mbalimbali, katika kusimama rasilimali fedha, rasilimali watu, jinsi gani unaongoza waliochini yako, hakika mafunzo haya yamekuja wakati muafaka na cha kufurahisha wahitimu wanatoka sekta mbalimbali za umma na sekta binafsi, tumechambua sera zote katika nchi yetu.Mafunzo haya yatatusaidia sana katika maeneo yetu ya kazi tunakoteka,'amesema Saada Mkuya Salum.
Amesema kila mhitimu baada ya mafunzo hayo watasaidiana na Serikali katika kuwatumikia wananchi na wanaamini wataacha alama katika utumishi wao. "Tunaamini tuliyopata hapa yatasaidia wengine kufikia malengo yao."
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment