Mageuzi ya kidigitali ulimwenguni yamerahisisha mawasiliano baina ya watu, hivyo kuibua fursa mpya za uchumi kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma na bidhaa mbali mbali.
Ukuaji huu wa teknologia pia umewezesha wanawake kuvuka mipaka na kuanza kushiriki kikamilifu katika shughuli rasmi na zisizo rasmi za kujitafutia kipato.
Bolt ni mfumo wa kuagiza usafiri kwa njia ya mtandao, unaowaruhusu wasafiri kutumia simu zao za mkononi popote walipo kuomba usafiri wa kuwafikisha popote pale wanapotaka kwenda.
Mfumo huu wa kidigitali umeondoa tofauti za kijinsia na kuwezesha wanawake kujiunga na kushiriki kikamilifu katika biashara ya usafirishaji. Bila kujali jinsia - dereva yeyote mwenye vigezo stahiki anaweza kupakua mfumo huu wa Bolt katika simu yake ya kiganjani, kujiunga na kuanza kutoa huduma za usafirishaji.
Mfumo wa Bolt unapunguza tofauti za kijinsia na kuwawezesha wanawake kujiongezea kipato. Umewafungua mlango ili wawe sehemu muhimu ya mfumo mpya wa uchumi unaojulikana kama uchumi wa kugawana, ambao nao umeibua aina mpya za ajira. Kwa pamoja, mageuzi ya kidigitali pamoja na uchumi wa kugawana zimewezesha wanawake wengi Zaidi kupata ajira zenye malipo ya papo kwa hapo.
“Kazi yangu ya udereva kupitia mfumo wa Bolt imenipa uhuru zaidi kiuchumi. Imebadilisha gari langu kuwa rasilimali muhimu ambayo inaniwezesha kujiongezea kipato. Hata siku zile ambazo biashara yangu nyingine inakosa wateja, bado nina uhakika wa kujipatia pesa kutokana na kusafirisha abiria,” dereva Esther Chali wa Dar es Salaam anasema.
Dada huyo mjasiriamali pia anamiliki mgahawa wa juisi ambapo ameajiri wasaidizi wawili. Anasema tangu ajiunge na mfumo wa Bolt, anafurahia uhakika wa kipato na uhuru unaomwezesha kujishugulisha na mambo mengi tofauti.
“Nimekuwa dereva kwa muda wa mwaka mmoja na nusu sasa. Mimi ni bosi wangu mwenyewe. Nachagua lini, wapi na kwa muda gani ninafanya kazi. Kipato change ni cha uhakika kwa sababu Bolt inanipa asilimia 85% ya nauli yote wanayolipa wasafiri wangu. Ni njia nzuri ya kupata hela bila wasiwasi wa makato yasiyoeleweka. Hali kadhalika naweza kujipatia fedha zaidi kwa kuwasaidia madereva wengine kujiunga na mfumo huu,” alisema.
Jamila Lada wa Dar es salaam ni dereva mwingine mwanamke anayenufaika na kipato kutokana na mfumo wa Bolt. “Zamani nilikuwa muuza samaki ila siku zote nilikuwa na hamu sana ya kuwa dereva. Daima nilihisi fursa kubwa ipo katika biashara ya usafiri ila sikuwa na uhakika jinsi gani ya kujiunga na fani hii,” mama huyo wa watoto watatu anasema.
Fursa yake kujiunga rasmi na kazi ya udereva ilijitokeza kupitia teknologia ya kuagiza usafiri kwa njia ya mtandao. “Nilikuwa natumia huduma za usafiri kwa njia ya mtandao ili kufanikisha biashara yangu ya zamani. Siku moja niliagiza usafiri na dereva aliyekuja kunichukua akawa ni mwanamke. Nilimuuliza maswali mengi sana kuhusu kazi yake na jinsi ya kujiunga. Mwishowe alinielekeza jinsi ya kujiunga na Bolt. Kwa bahati nzuri, aliniunganisha pia na mmiliki mmoja wa magari ambaye alikuwa anatafuta dereva na hapo ndio safari yangu kama dereva ilipoanzia,” anasema.
Jamila ambaye amekuwa dereva kwa mwaka mmoja sasa anasema kuwa kazi yake mpya ya udereva ni bora zaidi ikilinganishwa na biashara alizokuwa anazifanya hapo awali.
“Kazi hii ni rahisi kushinda ile ya kuchuuza samaki ambayo ilikuwa inanichosha sana na kuchukua muda wangu wote kudai madeni. Kwa sasa nimeamua kufunga biashara yangu ya samaki na kuweka juhudi zangu zote katika udereva. Nina matumaini ya kununua gari au hata pipipiki yangu mwenyewe ili niweze kujiajiri,” anasema.
Kuhusu usalama wake akiwa kazini, Jamila anasema kuwa hapo awali mume wake na baadhi ya wanajamii walikuwa na wasiwasi kuhusu usalama wake kama dereva mwanamke, hasa pale anapoamua kufanya kazi nyakati za usiku.
“Ila kwa sasa hawana hofu tena. Mfumo huu wa Bolt unatuunganisha madereva na abiria pia na huduma za dharura. Iwapo tatizo lolote likijitokeza wakati safari, dereva au abiria anaweza kubonyeza kitufe cha dharura (SOS) kwenye mfumo huu na moja kwa moja anapata msaada wa haraka,” anasema.
Bolt pia inashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo madereva, abiria, serikali na vyombo vyake vya ulinzi kudumisha usalama wa abiria na madereva.
“Naendesha kwa kujiamini kwa sababu ninajua kuwa mfumo huu unafuatilia kwa ukaribu mienendo yangu niwapo barabarani. Mteja pia anaweza kumruhusu mtu anayemwamini kufuatilia safari yake na kuona alipofika kwa njia ya simu. Kwa kweli mfumo huu umeongeza amani na utulivu kwa madereva, abiria na familia zetu kwa ujumla,” alisema Jamila.
Hizi ni baadhi tu ya mifano inayoonesha jinsi gani mfumo wa kuagiza usafiri kwa njia ya mtandao ulivyoondoa viunzi kwa wanawake kujiendesha ili waweze kuwa na uhuru kifedha.
Huku dunia yote ikielekea usawa wa jinsia, mifumo ya kuagiza usafiri kwa njia ya mtandao pamoja na ule wa biashara ya kugawana umeondoa baadhi ya changamoto zilizokuwa zinawazuia wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji wa mali.
Mfumo wa Bolt wa kuagiza usafiri kupitia mtandao umeibua fura za ajira na ujasiriamali ambao umewapa wanawake uhuru zaidi kifedha.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment