Na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv
OFISI ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam imetoa gari mbili kwa ajili ya kuzolea taka ngumu kwa ajili ya Manispaa ya Kigamboni.
akizungumza kwa niaba ya manispaa hiyo Meya wa Manispaa hiyo Meya wa Manispaa hiyo, Ernest Mafimbo kwa niaba ya Madiwani wa wa wilaya ya Kigambani ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa hekima aliyoionesha ya kuipatia Manispaa gari mbili za ukusanyaji taka ngumu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa magari hayo kwenye Ofisi za Mkurugenzi na Meya Amesema kuwa, Manispaa imepata nyenzo muhimu kwaajili ya kusafirisha taka ngumu kabla ya magari hayo hali ilikua mbaya na mrundikano wa taka ulikua ni mkubwa .
“Tunashukuru jitihada za Mkuu wa Mkoa kuhakikisha Kigamboni tunapata magari haya yatakayosaidia kuondoa taka ngumu kwa wakati, Uhitaji bado upo lakini kama Manispaa tunaendelea na jitihada zetu za kuhakikisha tunaongeza nyenzo nyingine ili zoezi la uwekaji mazingira safi liweze kutimia kwa kuwa na magari ya kuzoa taka ya kutosha” Amesema Meya.
Aidha Mstahiki Meya ametoa wito kwa wananchi kuacha kutupa taka hovyo na badala yake kuhifadhi taka hizo kwenye makasha yatakayowekwa kwenye maeneo yao ili kuweka mazingira safi.
Kwaupande wake Mkurugenzi wa Mansipaa Ndg.Erasto Kiwale amewashukuru Madiwai kwa kupokea magari hayo lakini pia ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni kwa jitihada walizozionesha kuhakikisha Kigamboni inapata magari ya kukusanyia Taka.
Mkurugenzi amesema jambo hilo limeonesha kuwajali wananchi na ameahidi kuwa magari hayo yatatumiwa vizuri katika kuweka mazingira safi huku akiwasisitiza wananchi kutunza vifaa hivyo na kuwata kuona kuwa suala la usafi ni la kila mtu sio kuitegemea Manispaa pekeyake.
Ameongeza kwa kusema kuwa makasha ya kukusanyia taka yatasambazwa kwenye maeneo yenye uzalishaji mkubwa ya taka ambayo ni Stendi ya mabasi Feri, Bandari Feri, Kwa Dumba Feri na Stendi ya mabasi Kibada ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati
Kupitia Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manispaa ya Kigamboni imewezeshwa kupata magari mawili ya kubebea makasha ya taka (skiploader) aina ya HOWO na makasha sita ya kukusanyia na kutunza taka.
Meya wa Manispaa ya Kigamboni,Ernest Mafimbo (katikati) kwa kusirikiana na Madiwani akikata utepe kuzinduwa magari ya kuzoa taka leo kwenye Ofisi za Mkurugenzi wilaya ya Kigamboni mkoa wa Dar es Salaam.kushoto Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni Erasto Kiwale.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment