Raisa Said,Tanga
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Amend iliyopo Jijini Tanga imezindua rasimu ya mpango mkakati wa usalama barabarani utakaolenga kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara
Afisa miradi kutoka Taasisi hiyo George Malekela alisema jana wakati wa uzinduzi wa rasimu hiyo kuwa lengo la mpango huo ni kutaka kuwalinda na kupunguza ajali za barabarani kwa watoto
Alisema kabla ya uzinduzi huo wa rasimu tayari walishaanza kufanya shughuli mbalimbali kama uboreshaji wa miundombinu ikiwa ni sehemu ya mradi huo , tangu mwaka jana jambo ambalo limeweza kupunguza ajali zilizokuwepo kwa watoto hasa katika maeneo ya shule ya msingi ,chuma,chuda na shule ya msingi masiwani.
Alisema mradi huo kwa sasa unafanyika katika shule za msingi na sekondari za Jijini Tanga ambapo utajikita katika kuboresha miundombinu, kutoa elimu elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi,kuanzisha klabu shuleni.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani cha jeshi la polisi Mkoa wa Tanga,Leopard Fungu alisema kuna vyanzo vitatu vinavyosabisha ajali nyingi kuwa ni tabia za kibinadamu,hali ya chombo chenyewe na mazingira ya barabara.
kuhusu hali ya usalama barabarani alisema kwa mwaka huu ajali tishio zimepungua ukilinganisha na mwaka jana ambapo ambapo mwaka jana kuanzia Januari hadi mach kulikuwa na ajali tishio 18 huku mwaka huu zikipungua hadi kufikia saba huku vifo vilivyotokea mwaka jana vilikuwa 16 na mwaka huu kipindi hicho kulikuwa na ajali tatu sawa na asilimia 81.5.
Alisema katika kipindi cha mwaka jana kuanzia Januari hadi machi watu 20 walikufa kwa ajali wakati kipindi kama hicho kwa mwaka huu waliokufa walikuwa ni watu watatu
Kwa upande wa ajali vifo vya pikipiki kifo ni wanafunzi (1), majeruhi ni (4) na kwamba hali hii imepungua kutokana na jitihada za Taasisi hiyo ya Amend ,vyombo vya habari pamoja na askali kutoa elimu katika vijiwe vya bodaboda na sehemu nyingine.
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kongamano hilo ni sehemu ya mpango unaofadhiliwa na Botnar Foundation ambao inatoa misaada wa kimaendeleo jijini hapa na lengo ni kuhakikisha ajali zinapungua.
Akifungua kikao cha kuzindua mpango wa Rasimu hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Mailapwa alisema umewasilishwa wakati muafaka na kwa sababu utasaidia kuwaepusha watoto wakiwamo wanafunzi na ajali ambazo zimekuwa zikitokea na nyingine kukatisha maisha yao.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment