Charles James, Michuzi TV
KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali za kutoa elimu bure, Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde amekabidhi mifuko ya Saruji 580 yenye thamani ya Sh Milioni 10 yenye lengo la kusaidia ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo kwenye Shule za Msingi na Sekondari ndani ya jimbo hilo.
Mbunge Mavunde amekabidhi mifuko hiyo kwa Afisa Elimu Msingi, Joseph Mabeyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ikiwa ni ahadi yake aliyoitoa muda mrefu ya kuendelea kukamilisha maeneo mengi yenye upungufu wa madarasa na yale ambayo hayakua na shule za msingi na sekondari.
Amesema Saruji hiyo aliyokabidhi itakwenda kutumika kama chachu katika maeneo hayo yote ambayo wanakwenda kuanza ujenzi wa shule za msingi na sekondari lakini pia kuongezea madarasa na matundu ya vyoo kwa shule ambazo zina upungufu.
" Nichukue fursa hii kuwapongeza Afisa Elimu Msingi na Sekondari kwa mchango wenu mnaoutoa kwenye sekta ya elimu na ndio maana na mimi nawiwa sana kuendelea kuchangia kwani napata mchango mkubwa kwenu, lengo letu ni kuendelea kutatua changamoto kwenye sekta ya elimu na mimi sitochoka kwani ndio kazi ambayo niliomba kwa wananchi.
Matumaini yangu ni kwamba ndani ya kipindi hiki kifupi tutakua tumeanza ujenzi wa Shule nyingi za Msingi na Sekondari, lengo langu ni kuwaona watoto wa Dodoma wanasoma katika mazingira rafiki.
Leo tumeanza na hatua ya kwanza ya kukabidhi Saruji hii yenye thamani ya Sh Milioni 10 lakini tutaendelea na utaratibu mwingine hatua kwa hatua na ninayo furaha kwamba zile fedha tulizoomba kwa Waziri Mkuu Sh Bilioni 1.9 sasa zitaanza kufanya kazi katika baadhi ya Shule kwenye Jiji letu la Dodoma na wanaanza ujenzi muda sio mrefu na pia kuna fedha zingine kama Milioni 46, 46 kwa zaidi ya Shule Nane katika Jimbo letu hili," Amesema Mavunde.
Ametoa rai kwa Madiwani wa Jiji la Dodoma kutumia Saruji hizo kama ilivyokusudiwa kwa kuwaandaa wananchi na yeye akiahidi kushirikiana nao kwa pamoja pindi ujenzi utakapoanza.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment