MWEKEZAJI wa Kiwanda cha Neel Salt, Ahmed Al Rawadh amesema kwamba yuko tayari kununua chumvi yote iliyopo kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara huku akisisitiza tangu kuzinduliwa kwa kiwanda chake cha chumvi amekuwa akitoa kipaumbele kwa wazalishaji chumvi wa mikoa hiyo.
Ametoa kauli hiyo katika kikao cha wadau na wazalishaji wa chumvi kilichofanyika mkoani Lindi baada ya kuwepo kwa malalamiko ya wazalishaji chumvi kwenye mikoa hiyo waliokuwa wakidai kuna chumvi nyingi kwenye maghala yao ambayo ni zaidi ya tani 250,000, jambo ambalo limebainika halina ukweli kwani baada ya kutakiwa kuthibitisha walishindwa kufanya hivyo.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Ahmed Al Rawadh amewaambia wazalishaji wa chumvi kuwa yupo tayari kununua chumvi yote ya wazalishaji hao wakati wowote na kwamba mzalishaji yoyote mwenye chumvi ghalani yupo tayari kuinunua.
Amesema kiwanda chake kinauwezo wa kusaga chumvi kilo 800,000 kwa siku na kuwataka wachimbaji wenye chumvi ghafi kwenda kiwandani kwake muda wowote kupeleka mzigo huo ."Nimeshatoa maelekezo kwa wasaidizi wangu kuwa wazalishaji wa chumvi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wakifika kiwandani wahudumiwe haraka iwezekanavyo ili warudi walipotoka na kuendelee na majukumu yao,"amesema Ahmed
Kuhusu ubora, Mkurugenzi huyo ametoa upendeleo kwa wachimbaji wa chumvi wa mikoa ya Lindi na Mwara kwenda shambani kwake kujifunza shamba darasa ili wapate chumvi yenye ubora kwani japo ana kiwanda pia anamiliki shamba lenye hekari 2500.
Akizungumzia kuagiza chumvi nje ya nchi amekiri kweli amekuwa akiagiza chumvi nje ya nchi kwa kibali na Serikali ili kukidhi mahitaji ya bidhaa hiyo nchini baada ya kuwasiliana na viongozi wa wazalishaji chumvi ghafi.
Kwa upande wake Ofisa Madini wa Mkoa wa Lindi Idd Msikozi, ameonesha kusikitishwa na taarifa hizo zisizo na ukweli za uwepo wa chumvi ghafi kwenye maghala yao kiasi hicho na kuagiza kuanzia sasa wazalishaji wote wanatakiwa kujaza taarifa za uchimbaji wao ili Tume ya Madini iwe na taarifa za wachimbaji wote za kila mwezi kwa lengo la kujua mkoa wa lindi una kiasi gani cha chumvi ghafi.
Amesema kitendo cha ofisi yake kutokuwa na taarifa sahihi na atakayeshindwa fanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa na kwamba wazalishaji hao miaka yote wanakuwa wanalakamika kuwa chumvi wanayouza ni bei ndogo.
Msikozi amefafanua hata mrabaha wanaolipa selikalini ni kidogo, hivyo leo amefika mwekezaji huyo kununua chumvi yote lakini ado wanasigana kuhusu bei sasa
"Tunaunda kikosi kazi kutembelea wachimbaji wote kukagua maghala na mashamba na tukikuta kuna taarifa tofauti na zile tulizojaza kwenye fomu za tume ya madini basi tutakuwa hatuna msamaha na yoyote yule,"amesema Msikozi
Aidha Ofisa madini huyo amesema pindi mnunuzi anapokuja kutaka kununua madini hayo ya chumvi inakuwa ngumu kupata idadi kamili ya mali iliyopo." Mkurugenzi wa kiwanda hiki atanunua chumvi yoyote iwe nyeupe,nyeusi au bluu.
" Ila yenye mchanga hawezi kununua kikubwa tunawaomba wachimbaji kuwa waaminifu kwani wengine wanachanganya chumvi na mchanga ili uzito uongezeke."
Wakati huo huo Mmoja wa wachimbaji wa chumvi kutoka wilaya ya kilwa mkoani lindi Ahmed Mjaka alikiri kuwa kulikiwepo na sintofahamu baina ya wachimbaji na uongozi wa kiwanda hicho lakini baada ya kikao hicho cha wadau wamefikia makubaliano ya kuuza chumvi yao kwa mwekezaji huyo kati ya Sh.8000 kwa bei ya shambani na Sh.10,000 kwa bei ya kiwandani.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment