UZINDUZI WA USHIRIKIANO WA HUDUMA ZA KIFEDHA KATI YA PBZ BANK NA AIRTEL (AIRTEL MONEY) | Tarimo Blog

Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa kushirikiana na mtandao wa simu wa AIRTEL (AIRTEL MONEY), leo katika ofisi kuu za benki hiyo iliopo Mpirani Zanzibar, wamezindua huduma ya ushirikiano wa miamala ya kifedha katika kulenga kumrahisishia na kumsogezea mteja huduma karibu yake wakati wote na popote pale alipo nchini. Huduma hii kwa kushirikiana na Airtel Money itamuwezesha mteja wa PBZ benki kufanya miamala ya kifedha kwa urahisi bila usumbufu wala foleni.

Akiongea kutokea Zanzibar, katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Bw Dkt Muhsin Salim Masoud, amesema Bank ya Watu wa Zanzibar mara kwa mara hubuni mambo tofauti tofauti mazuri yanayolenga kuwahudumia wateja wao kwa unafuu na ubora zaidi. 

Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) amesema ushirikiano huo pamoja na kumsaidia mteja pia inalenga kuakisi sera za kifedha za nchi juu ya uchumi jumuishi, sambamba na kuunga mkono kasi ya kimaendeleo inayooneshwa kivitendo na viongozi wetu wakuu wa nchi, Mhe. Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Dr. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kuwahudumia wananchi katika hali ya ubora zaidi.

Kupitia ushirikiano huo mawakala na wateja wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na wale wa Aitel (Airtel Money) wataweza kufanya miamala ya huduma za kifedha kwa urahisi, salama na kwa haraka katika kuyafikia mahitaji yao. 

Mawakala wa Airtel Money kwa fursa hii ambao ni wateja wa Benki ya Watu wa Zanzibar, wataweza kujihamishia fedha kirahisi aidha kutoka PBZ kwenda Airtel Money au kutoka Airtel Money kwenda PBZ na kuweza kuendelea na huduma zao pasina kuhangaika huku na kule kwa lengo la kupata floats (salio)

Jinsi ya kupata huduma hiyo mteja wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kupitia simu yake ya mkononi (simu janja na za kawaida) atapiga *150*40# halafu atachaguwa #2 halafu atachaguwa #4 halafu atachaguwa #6 kuweza kutuma fedha kutoka PBZ benki kwenda Airtel Money. Huduma hii pia inaweza kupatikana kupitia PBZ Mobile App (ambayo unaweza kuipata kupitia Play Store) na PBZ Internet Banking.

Nae Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema Zanzibar “Airtel tunaunganisha nguvu leo na wenzetu wa benki ya Watu wa Zanzibar ili kuhakikisha kuwa wateja wanapata huduma za kifedha kidigitali. Ushirikiano wetu huu utawafanya wateja wetu hapa zanziba na maeneo mengine kupata huduma za kibenki kwa urahisi sana.

Naomba nitoe rai kwa wateja wa Airtel Money pamoja na Mawakala kutumia hii fursa kwani ni njia salama, rahisi na nafuu”. Nchunda alisema.

Tunaelewa kwamba mawakala wa Airtel Money ni wafanya biashara kama walivyo wafanya biashara wengine ambao wanahitaji uhakika wa upatikanaji wa fedha muda wote na kuokoa muda. Kwa kuzindua ushirikiano wetu huu, tunawahakikishia Mawakala uhakika kufurahia kutumia mtandao wetu kwa kufanya chaguo la huduma zao wakiwa popote na kupata fedha muda wote.

“Kwa sasa tunaishi kwenye dunia ambayo malipo yanafanyika kila sekunde kupitia simu za mkononi, hivyo ubia wetu na benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) utatusaidia sisi kufanikisha lengo letu la kutoa huduma zenye ubunifu wa hali ya juu, unafuu na hivyo kukidhi mahitaji ya kila siku ya wateja wetu

Na ili mteja wa Airtel Money aweze kufurahia ushirikiano huu, hatua zifuatazo ni muhimu Piga *150*60# ili kupata menu ya Airtel Money, Changua 1 kutuma fedha, Changua 4 kutuma kwenda benki kisha Changua benki yako.

Kwa sasa, Airtel Money Tanzania imeunganishwa kwenye malipo ya bili zaidi ya 1000 pamoja na taasisi za kifedha Zaidi 40 ambapo mteja anaweza kutoa na kuweka fedha. Vile vile, Airtel Tanzania inaendelea kutanua wingo wa huduma za Airtel Money ambapo kwa sasa tunao Airtel Money Branches Zaidi ya 800 ambazo zinatoa huduma na bidha za Airtel.


Mkurugenzi Mtendaji Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), Dkt Muhsin Salim Masoud (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda wakionyesha bango baada ya kuzindua ushirikiano wa miamala ya kifedha katika kulenga kumrahisishia na kumsogezea mteja huduma karibu yake wakati wote na popote pale alipo nchini. Huduma hii kwa kushirikiana na Airtel Money itamuwezesha mteja wa PBZ benki kufanya miamala ya kifedha kwa urahisi bila usumbufu wala foleni.

Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda akiongea mjini Zanzibar baada ya kuzindua ushirikiano na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ), ushirikiano huo wa miamala ya kifedha unalenga kumrahisishia na kumsogezea mteja huduma karibu yake wakati wote na popote pale alipo nchini. Huduma hii kwa kushirikiana na Airtel Money itamuwezesha mteja wa PBZ benki kufanya miamala ya kifedha kwa urahisi bila usumbufu wala foleni.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2