SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewataka wabunge kutovaa tai nyekundu, wakati wa kikao cha saa 10:00 jioni ya leo ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan atalihutubia Bunge kwa mara ya kwanza tangu kuapishwa kwake.
“Napenda kuwakumbusha waheshimiwa wabunge leo anapokuja kiongozi mkuu wa nchi Bungeni basi haishauriwi sana kuvaa tai nyekundu, Nafikiri tunakubaliana red inabakia na wenye mamlaka, kwa hiyo ni vizuri kuyajua haya mambo baadae jioni tutakapo rudi, ukivaa tai nyekundu utarudia getini” amesema spika Ndugai.
Leo Aprili 22 majira ya saa 10:00 jioni, Rais Samia Suluhu Hassan atalihutubia bunge la Tanzania kwa mara ya kwanza tangu aapishwe Machi 19,2021.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment