PINDA AMUOMBEA KURA ZA UENYEKITI WA CCM RAIS SAMIA "AMEPANGWA NA MUNGU" | Tarimo Blog

 








Charles James, Michuzi TV

WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mizengo Pinda amewataka wajumbe 1876 wanaoshiriki mkutano mkuu maalum wa Chama cha Mapinduzi kumchagua kwa kishindo Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Sita wa CCM.

Pinda amesema uzoefu wa miaka 34 wa kuwa Mwanachama wa CCM na uzoefu wa miaka 44 akiwa mtumishi wa Serikali vinatosha kumfanya kuwa mwenye sifa na uwezo wa kukiongoza Chama hicho.

Amesema uwezo wake aliouonesha wa kufanya kazi kama Makamu wa Rais chini ya Dk John Magufuli vimemfanya amuamini kwamba anatosha kuwa Mwenyekiti wa chama hicho kinachotawala.

" Ameondoka Dk Magufuli akiwa na miaka 61 na Mama Samia ameapishwa Machi 19 kuwa Rais akiwa na miaka 61 kumbe hili jambo limepangwa na Mungu, tumpigie kura zote za ndio ili tumpe moyo na nguvu ya kuendeleza kazi iliyoachwa na Dk Magufuli.

Alivyofariki Dk Magufuli yakazuka maneno ya hapa na pale lakini Mama mwenyewe akasema yeye na Hayati ni kitu kimoja, hivyo niwasihi wote tumpigie kura Rais Samia kuwa Mwenyekiti, nitashangaa kama baada ya kazi yote hiyo tutapata matokeo tofauti na asilimia 100," Amesema Pinda.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2