RAIS SAMIA KUWEKA REKODI YA TATU KWENYE HISTORIA YA TANZANIA | Tarimo Blog

 





Charles James, Michuzi TV

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM, Philip Mangula amesema kazi kubwa iliyofanywa na wagombea wao wa Urais na Umakamu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ndio iliyosabisha chama hicho kipate heshima kwa wananchi.

Kupitishwa kwa Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa CCM kunamfanya kuweka rekodi tatu muhimu katika historia ya Nchi yetu toka kupata kwa Uhuru Desemba 9, 1961.

Rekodi hizo ni za kuwa Makamu wa Rais wa kwanza Mwanamke mwaka 2015 hadi 2021. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo aliapishwa Machi 19 mwaka huu na sasa leo anathibitishwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza Mwanamke wa CCM.

Mangula ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua mkutano maalum wa chama hicho wenye ajenda moja tu ya kulipitisha jina la Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Sita wa CCM.

Rais Mama Samia anapigiwa kura za kupitishwa kuwa Mwenyekiti wa CCM kufuatia kifo cha aliyekua Rais na Mwenyekiti wa chama hicho, Hayati Dk John Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu.

Wajumbe 1876 kutoka kila Wilaya ya Tanzania wamefika jijini Dodoma tayari kulithibitisha jina la Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2