Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV - Dodoma
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema yeye sambamba na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli walikuwa kitu kimoja katika kutekeleza yale yote yaliahidiwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyokuwa ikinadiwa wakati wa Kampeni za Uchaguzi mwaka 2015 na 2020.
Akizungumza jijini Dodoma wakati akihutubia Bunge tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia amezishukuru awamu zote Tano za Uongozi katika mafanikio ya Taifa la Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika awamu zote Nane za Uongozi kwa kudumisha ustawi na maendeleo ya watu wa Zanzibar.
Aidha, Rais Samia amesema dira na muelekeo wa Serikali ya awamu ya Sita ni pamoja na kudumisha awamu zote zilizopita kwa kuendeleza yale yote mazuri na kuleta mengine mapya yatakayoleta tija kwa taifa la Tanzania.
Pia Rais Samia amewashukuru watangizi wake, akiwemo Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Amani Abeid Karume, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment