RAIS SAMIA AAHIDI SERIKALI YAKE KUYAENZI MAZURI YOTE YALIYOFANYWA NA WATANGULIZI WAKE | Tarimo Blog

Charles James, Michuzi TV

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema serikali yake anayoiongoza ya awamu ya sita itaendeleza na kuyaenzi mazuri yote ambayo yalifanywa na serikali za awamu zilizopita kuanzia awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere hadi ya mtangulizi wake, Dk John Magufuli.

Rais Samia ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akihutubia Bunge hilo ambapo amesema licha ya kuenzi mazuri hayo pia watafanya mabadiliko kwa lengo la kuongeza tija na ufanisi zaidi.

Amesema dira na muelekeo wa serikali yake ni kudumisha mazuri ya awamu zilizopita na huo ndio msingi haswa wa kauli mbiu yake ya "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi Iendelee".

" Nizipongeze awamu zote zilizopita kwa kufanya kazi kubwa ya kuwahudumia watanzania, hivyo niseme mambo ambayo tutayafanya ni yaleyale ambayo yalisemwa na Rais aliyepita Hayati Dk John Magufuli kwani wote tulishiriki kuinadi Ilani ya Chama chetu cha CCM mwaka 2020 na ndio maana nilisema sisi ni wamoja.

Serikali yetu ya awamu ya sita itaendelea kudumisha na kulinda tunu za Taifa letu ambazo ni Amani, Umoja, Mshikamano, Muungano wetu na Mapinduzi ya Zanzibar," Amesema Rais Samia.

Amesema serikali ya awamu ya sita katika miaka mitano hii haitovumilia uzembe, wizi, rushwa na ubashirifu katika eneo lolote.

Kuhusu ukuaji wa uchumi, Rais Samia amesema serikali yake itachukua hatua stahiki za kurudisha imani kwa wawekezaji nchini pamoja na kuwezesha uwekezaji kufanyika kwa haraka.


 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2