RAIS SAMIA: TUTALILEA SHIRIKA LETU LA NDEGE KWA KULIONDOLEA MADENI NA TOZO | Tarimo Blog

Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuboresha sekta ya usafiri wa anga nchini, Serikali imepanga kulilea Shirika la Ndege kimkakati ili liweze kujiendesha na kukua lenyewe na kuweka mahesabu yake sawa.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Rais Samia Suluhu Hassan wakati akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amesema katika kulilea Shirika hilo wamepanga kuliondolea tozo na madeni iliyonayo.

Rais Samia amesema Shirika hilo limekua likionekana halina thamani na linajiendesha kwa hasara kwa sababu ya kuwa na madeni mengi ambayo wamekua yakirithiwa kwa muda mrefu.

" Kwa sasa Shirika letu linaonekana halina thamani kwa kuwa limethiri madeni mengi ya nyuma, hatutokubali kuona shirika letu linapata hasara ilihali tumelifanyia Uwekezaji mkubwa.

Tunaenda kufanya uchambuzi wa kina kuona namna gani ya kuliendesha kwa faida Shirika letu kwa kuwa na rasilimali watu bora tena tuliowachunguza na kuwaamini," Amesema Rais Samia.

Akizungumzia sekta ya Utalii, Rais Samia amesema serikali ya awamu ya sita imepanga kuwekeza katika Utalii wa mikutano, fukwe na malikale lengo likiwa ni kuongeza idadi ya watalii watakaotembelea vivutio vyetu nchini pamoja na mapato ya sekta hiyo kutoka Sh Bilioni 2.6 hadi Bilioni Sita.

" Katika kukuza sekta hii pia tumepanga kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza kwenye sekta hii kwa kujenga mahoteli na pia kama serikali kusomesha vijana wetu ili kupunguza kutegemea wataalamu kutoka nje ya Nchi, " Amesema Rais Samia.


 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2