Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kuwaapisha MAkatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi Ikulu jijini Dar es salaam leo Jumanne April 6, 2021
*Asema bango moja la mwananchi litaondoka na Mkurugenzi au Mkuu wa Wilaya
*Asisitiza umuhimu wa kukusanya kodi bila mabavu, ampa malekezo kamisha TRA
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa muelekezo wa Serikali kwa kufafanua masuala mbalimbali huku akitwumia nafasi hiyo kusisitiza watendaji na watumishi wa Umma kuhakikisha wanatimiza majukumu yao.
Katika kusisitiza utendaji kazi Rais Samia ametumia msemo wa kwamba anachotaka ni watu kufanya kazi na iwapo watazingua basi watazinguana na kwamba anapotumia neno anaomba wajue kabisa ndio anatoa maagizo na maelekezo.
Rais Samia amesema hayo leo Aprili 6 mwaka 2021 baada ya kuwaapisha Makatibu na Manaibu Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali.Aidha amewaapisha baadhi ya Makamishna na wakurugenzi wa Taasisi na Mamalaka za Serikali.
Kuhusu suala la haki, Rais Samia amesema kwamba nie vama watendaji na watumishi wa umma wakatenda haki katika kuwatumia wananchi kwani ameshuhudia ziara za viongozi ambapo kuna mabango mengi yanayozungumzia changamoto za watu.
"Haki za wananchi, tunapokwenda kwenye ziara tunapokelewa na mabango na mabango mengi yanayonekana yanayozungumzwa ni yale ambayo yanaweza kushughulikiwa, bango moja aidha Mkurugenzi au Mkuu wa Wilaya ataondoka.Nataka kusema hii isiwe sababu ya kuzuia wananchi wasioneshe mabango yao.
"Tukipata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wamezuiwa kuonesha mabango yao kwa viongozi tutachukua hatua.Shughulikieni changamoto za wananchi kwenye maeneo yenu,"amesema Rais Samia wakati akizungumzia utoaji haki kwa wananchi.
Kuhusu TAMISEMI, Rais Samia ametumia nafasi hiyo kufafanua mambo mbalimbali katika kuhakikisha TAMISEMI inaendelea kuwatumikia wananchi ambapo amewasisitiza kukusanya kodi."Tunaomba mkakusanye kodi, TAMISEMI mkahakikishe mnakwenda kukusanya kodi, Wizara kwa ujumla na TAMISEMI niwaombe muendelee kwenda kusimamia ukusanyaji huo.
"Katika Ofisi ya Waziri Mkuu kulikuwa na makatibu wakuu wawili au watatu, sasa nimeamua kupunguza na kuwa a Katibu Mkuu mmoja na Manaibu wawili, mwanzo ilikuwa changamoto nani awe ofisa masuhuli.Pia katika Ofisi ya Waziri Mkuu kuna ofisi binafsi ya Waziri Mkuu fedha aliyokuwa anapelekewa ilikuwa inakatwa, hii si heshima, naagiza fedha kwa ajili ya ofisi hiyo isikatwe,"amesema Rais Samia.
Kuhusu vibali vya kazi ambavyo vinatolewa kwa waekezaji wanaokuja nchini, amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika utoaji wa vibali vya kazi.Vibali vya kazi hapa kumekuwa na manyanyaso, ndipo eneo ambalo watu wanatumia kuchuma fedha, anaomba kibali fedha zinamtoka.
"Vibali vya kazi vimekuwa na changamoto, mtu anakuja na mradi binafsi anataka kuweka mtu wake, mnasema hapana, tunaka mtu afurahie uwekezaji wa Tanzania, kampuni zinafungwa na watu wanaondoka, kampuni zikifugwa na fedha zinaondoka na ndio kilio cha watanzania mifukoni mitupu.Kama kuna mtu anataka kuja kuwekeza na ana watu wake kwanini akatazwe na ndio anayemuamini, acheni urasimu katika kutoa vibali, tunataka watu waje kuwekeza,"amesisitiza.
Akifafanua zaidi amesema katika ofisi ya Waziri Mkuu kuna uwekezaji,hivyo ameagiza kuwepo na eneo moja ambalo kuna huduma zote, kwani nako kuna urasimu mkubwa."Hakuna wa kufanya maamuzi, kuna mzunguko mkubwa , hakuna mawasiliano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaaa, naomba mnaosimamia uwekezaji nendeni mkae huko muondoke urasimu huu.
Akifafanua zaidi amesema katika ofisi ya Waziri Mkuu kuna uwekezaji,hivyo ameagiza kuwepo na eneo moja ambalo kuna huduma zote, kwani nako kuna urasimu mkubwa."Hakuna wa kufanya maamuzi, kuna mzunguko mkubwa , hakuna mawasiliano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaaa, naomba mnaosimamia uwekezaji nendeni mkae huko muondoke urasimu huu.
"Lakini lingine ni kodi kwa wawekezaji, hakuna uwiano kuhusu kodi, tumevishwa chapa kwamba Tanzania hatutabiriki, naagiza mkanyooshe haya.Juzi tu nilitoa kauli kuhusu kodi, nimepokea simu nyingi, naomba tuvute tena uwekezaji tupate kodi,"amesema.
Amesisitiza umuhimu wa kupunguza misuli kwenye eneo hilo la kodi."Sisi tunahitaji zaidi uwekezaji lazima tuangalie vizuri, tukafanye kazi, tukarudishe imani ya wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania.Pia naomba mifumo ya fedha ikaangaliwe upya, lazima tujue mifumo yetu ya kukusanya fedha ni ipi."
Amesisitiza umuhimu wa kupunguza misuli kwenye eneo hilo la kodi."Sisi tunahitaji zaidi uwekezaji lazima tuangalie vizuri, tukafanye kazi, tukarudishe imani ya wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania.Pia naomba mifumo ya fedha ikaangaliwe upya, lazima tujue mifumo yetu ya kukusanya fedha ni ipi."
Akizungumzia miradi ya vipaumbele , amesema kuna urithi wa miradi ambayo wameachiwa na Rais Hayati Dk.John Magufuli ambayo lazima itekelezwe na kukamilika kama ilivyokusidiwa."Tuna mirathi ambayo tumeachiwa na aliyekuwa Rais wetu, naomba sana sana twende tukasimamie miradi hiyo ya kimkakati.
"Kumuwepo na ucheleweshaji wa malipo tena kwa makusudi tu, kuna kipengele kinachozungumzia riba iwapo malipo yatachelewa, kinachoonekana wanaochelewesha malipo maana yake kuna mazungumzo hapo kati kati. Tunaongeza gharama za miradi, watu wa fedha nendeni mkasimmamie miradi iendelee vizuri."
Kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje, Rais Samia amesema ameteua Waziri mwanamama Shupavu pamoja na Katibu Mkuu wake ambaye anaijua vizuri Wizara hiyo, hivyo ni matarajio yake watakwenda kukuza mahusiano kati yetu na mataifa ya nje."Wizara ya Mambo ya Nje mnafanya kazi kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ni pande zote za muungano. Hakuna haja ya kuwekeana vigingi."
"Kumuwepo na ucheleweshaji wa malipo tena kwa makusudi tu, kuna kipengele kinachozungumzia riba iwapo malipo yatachelewa, kinachoonekana wanaochelewesha malipo maana yake kuna mazungumzo hapo kati kati. Tunaongeza gharama za miradi, watu wa fedha nendeni mkasimmamie miradi iendelee vizuri."
Kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje, Rais Samia amesema ameteua Waziri mwanamama Shupavu pamoja na Katibu Mkuu wake ambaye anaijua vizuri Wizara hiyo, hivyo ni matarajio yake watakwenda kukuza mahusiano kati yetu na mataifa ya nje."Wizara ya Mambo ya Nje mnafanya kazi kwa ajili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ni pande zote za muungano. Hakuna haja ya kuwekeana vigingi."
Akizungumzia Tanzania ya viwanda, Rais Samia amesema lazima Tanzania ya viwanda iwe inaeleweka kwa watu, viwanda vingi vinakwenda mkoani na wilayani, hivyo lazima kuwe na utaratibu wa kuwa na kanzu data ya kufuatilia maendeleo ya viwanda hivyo vilipo na mwenendo wao.Aidha amezungumzia umuhimu wa kuendelea kutafuta masoko yakiwemo ya mazao yanayozalishwa nchini.
Kwa upande wa madini ,Rais Samia amesema kuna haja ya kufanyika kwa majadiliano katika kuhakikisha madini yaliyopo nchini yaachimbwa na kuwanufaisha Watanzania wote."Kwenye madini najua tuna ubia na kampuni za nje, najua Barick tunashirikiana nao kupitia kampuni ya Twiga.Katika eneo hili la madini kama kuna kodi za kusamehe tusamehe.
"Kwenye mazungumzo yafanyike mapema kupita Kamati za majadiliano ili tuanze kufanya kazi na nchi ifaidike.Uchimbaji maeneo ya hifadhi, najua kuna madini katika maeneo ya TANAPA , madini yachimbwe maana hata yakikaa kwenye hifadhi tembo hawali madini.
"Mirerani tumejenga ukuta , tumeweka na majeshi lakini madini yanatoka kama mwanzo, tukabaini madini ndio utanaota yanapigwa picha na Rais, tuweke udhibiti katika madini, yanaendelea kuibwa.
"Lakini kwenye kitalu C sitaki kuona mkono wa mtu, wapo walianza kugawa kile kitalu waache, kuna matumizi yake,"amesema na kuongeza "Madini yetu ndio tegemeo letu kwenye nchi, tusiposimamia vizuri tunashusha uchumi wetu, simamieni vizuri.
Kwa upande wa Wizara ya Ardhi, Rais Samia amesema bado kuna dhuluma kubwa ambayo inafanyika katika kudhulum ardhi za watu na baadhi wanaofanya dhuluma hiyo na maofisa ardhi, hivyo ameagiza eneo hilo liangaliwe kwa umakini.
Wakati katika Wizara ya Maji, amesema iwe mvua, iwe jua lazima maji yapatikane asilimia 95 kwa mijini na asilimia 85 kwa maeneo ya vijijini."Mtakwenda kufanya nini mtajua wenyewe, lakini ikifika mwaka 2025 maji lazima yapatikane kwa kiwango kinachotakiwa, tunadeni kubwa kwa wananchi kwenye maji"
Katika Wizara ya Habari, Sanaa ,Utamaduni na Michezo , ametoa maagizo kuhakikisha vyombo vya habari ambavyo vimefungiwa na hasa televisheni za mtandaoni, zifunguliwe lakini sheria na kanuni zifuatwe na adhabu ambazo zitatolewa ziwe wazi ili kila mmoja ajue.
Aidha amesema kuna haja ya kuwekwa kwa mazingira mazuri kwa wasanii na wanamichezo kwani ni eneo ambalo linaajiri wananchi wengi.Pamoja na hayo amesisitiza umuhimu wa maeneo yote ya utumishi wa umma kutimiza majukumu yake huku akitumia msemo kwamba yeye ni Mama lakini atakayezingua basi watazinguana.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment