SERIKALI IMEENDELEA KUTEKELEZA MKAKATI WA MIAKA MITANO WA KUTEKELEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO. | Tarimo Blog


 Na Jusline Marco-Arusha

Serikali imeendelea kutekeleza mpango mkakati wa miaka mitano wa kitaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kipitia mpango kazi wa miaka 5 ulioanza kutekelezwa mwaka 2017/18 na utahitimishwa mwaka 2021/2022.

Kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kwa kushirikiana na TAMISEMI kimeendelea kuwajengea uwezo maafisa ustawi wa jamii nchini  ili kuweza kulinda na kutetea  haki za makundi maalum wakiwemo wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

Akifungua mafunzo hayo mkurugenzi huduma za ustawi wa jamii kutoka ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Rasheed Maftah alisema kuwa serikali ina sera na mikakati mbalimbali inayoitekeleza ili kupambana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa miaka mitano ambao umeanza mwaka 2021 hadi 2022.

"Tunataka hadi kumalizika kwa mkakati huo tuwe tumetokomeza ukatili kwa watoto kwa asilimia 50 kwani pamoja na jitihada zote tunazozifanya bado kuna changamoto ikiwemo mimba za utotoni,"Alisema Maftah.

Alieleza wanatekeleza mkakati wa miaka mitani wa kutokomeza ulatili  ambapo hadi hivi sasa wameshaanzisha kamati za ulinzi na usalama  wa  watoto na wanawake mikoa yote na katika halmashauri zote 184 pamoja na ngazi za kata vijiji na mitaa ambazo zimekuea niza msaada sana dhidi ya ukatili.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Bi.Anna Henga alisema kuwa kituo hicho kimeweka mpango mkakati namba nne wa kulinda na kutetea haki za makundi maalumu wakiwemo wanawake,watoto na watu wenye ulemavu ambapo alisema makundi hayobyameendelea kupitia changamoto mbalimbali duniani na nchini Tanzania hali iliyopelekea kutofurahia haki zao.

Aliongeza kuwa ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2020 inayoandaliwa na kituo cha sheria na haki za binadamu imeripoti kuwa kesi zaidi ya elfu 26544 za ukatili kwa wanawake ikiwemo vifo 32 vya wanawake kuuawa na wenza wao huku akitaja kanda zinazoongoza kuwa ni pamoja na Kanda ya ziwa,Kanda ya Magharibi na kanda ya mashariki.

"Ripoti hiyo imeripoti zaidi ya kesi 7263 za ubakaji kwa wanawake katika mikoa ya Dar es salaam,Kilimanjaro,Tanga,Mbeya na Dodoma huku katika mwaka 2019 ripiti hiyo imesema zaidi ya kesi elfu 4397 za ukatili wa kingono kwa watoto zimeripotiwa Alisema Bi.Henga

Vilevile alieleza kuwa kumekuwa na ongezeko la ukatili wa kimwili,ndoa za utotoni pamoja na ukeketaji ambapo mikoa iliyoripotiwa kuongoza kwa ukatili wa watoto kuea ni Shinyanga, Tabora, Mara, Lindi na Mirogoro ambapo kituo kimekuwa kikihakikisha haki za binadamu zinaheshimiwa nchini Tanzania kwa kutoa elimu ya haki za binadamu,kuwajengea uwezo watu kuhusu sheria na haki za binadamu.

Pamoja na hayo Bi.Anna alieleza kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali za utekelezaji na ulinzi wa watoto wanaokinzana na sheria, watoto wanaoingiliana na sheria huku wengine wakiathiriwa na ukatikili ambapo upatikanaji wa haki umekuwa changamoto hivyo nu muhimu kwa maafisa ustawi kujengewa uwezo wa kutambua sheria ,miongozi namienendo ya ulinzi wa haki za watoto ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Jahnson Lukindo kutoka Mkoani Kilimanjaro ambaye anasimamia masuala ya uendeshaji wa kesi mahakamani kwa makundi maalum na watoto alisema kuwa mafunzo hayo yatawapa uimara wa kusimamia kesi zinazohusu watoto pamoja na walemavu  ili kuhakikisha makundi hayo yanapata haki zao.

Aliongeza kuwa wazazi kumalizana kinyumbani ni moja ya changamoto ambazo husababisha ukatili dhidi ya watoto na wanawake kuendelea kushamiri katika baadhi ya mikoa ambapo wameendelea kujitahidi kutoa elomu mara kwa mara kipitia mikutano ya vijiji, makanisani na misikitini oli kuweza kuondoa tatizo la elimu duni kwa wana jamii.

Faithmerry Lukindo mmoja wa washiriki hao kutoka Mkoani Mwanza alieleza kuwa mila potofu, malezi ya kambo  watoto kuishi mitaani pamoja na kukosekana kwa maadili katika  jamii ni moja ya vitendo vya kikatili kuendelea kushamiri katika jamii.

Faithmerry Lukindo mshiriki katika mafunzo ya maafisa ustawi wa jamii yaliyofanyika jijini Arusha.
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu Anna Henga akitoa ripoti za hali ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto zolizofanywa na kituo hicho
Johnson Mndeme msimamizi masuala ya uendeshaji wa kesi mahakamani wilayani Same,Mkoami Kilimanjaro akieleza changamoto zilizopo katika wilaya hiyo dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto.
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2