BODI ya Shirikisho la Muziki Tanzania katika Kikao chake cha Tarehe 12 April 2021 kiliazimia kwa kauli moja kuunda kamati itakayoratibu mchakato wa kumpata Katibu Mkuu wa Shirikisho la Muziki Tanzania.
Kamati hiyo imepewa jukumu la kutafuta Katibu Mkuu mwenye kubeba Sura ya Muziki wa Tanzania, anayejua changamoto za Wanamuziki Tanzania, anayejiweza kiakili na maarifa kuhakikisha kuwa Shirikisho linaachana na Utegemezi wa Kiuchumi na hivyo kujitegemea, Katibu Mkuu ambaye ana uhusiano na watu wote hivyo kuwaunganisha wadau wote wa Muziki Tanzania.. Katibu Mkuu atayeunda Kamati za Shirikisho la Muziki zitakazosaidia kufikia malengo makuu ya Shirikisho la Muziki, Katibu Mkuu ambaye ni Muumini wa Umoja na Mshikamano pamoja kuongozwa na Staha bila woga katika kuongoza wanamuziki wote.
Anayetakiwa ni Katibu Mkuu ambaye ataunganisha Wanamuziki na Serikali pamoja na wadau wengine wa Muziki katika kutetea na kulinda Maslahi ya Wanamuziki na Tasnia ya Muziki kwa Ujumla. Katibu Mkuu ambaye atashirikiana na vyama vyote vinavyounda Shirikisho la Muziki Tanzania kuhakikisha kuwa kunakuwepo Mshikamano, Katibu Mkuu atayekuza mahusiano kati ya Shirikisho la Muziki na Wadau wa Habari, COSOTA, BASATA, WIZARA NA TAASISI ZA SERIKALI NA ASASI mbalimbali kuleta maendeleo ya wanamuziki, Katibu Mkuu ambaye atasaidia wadau mbalimbali kama vile wadhamini kuwezesha kusogeza mbele majukumu ya Shirikisho na kuwawezesha wadau hao kuwa sehemu muhimu ya maendeleo. Katibu Mkuu ambaye anaendana na muda na wakati huu tulionao. Katibu Mkuu atakaa kupindi chote cha miaka mitano ambayo imeanza mwezi Machi 2021 wakati viongozi wapya walipochaguliwa. Katibu Mkuu anayejua changamoto za Wanamuziki na njia ya kuzitatua kwa kushirikiana na bodi na wadau mbalimbali.
Mtu mwenye sifa hizo anaweza kupendekezwa na Vyama vinavyounda Shirikisho, Wadau Mmoja mmoja au yeye mwenyewe binafsi kwa kuonesha nia hiyo kwa kuwasiliana na wafuatao Viongozi wafuatao,
Addo November (Rais) 0718500000
Mzee Yusuf (Makamu wa Rais)
+255655888889
Siza Mazongera( Katibu wa Uenezi ) +255713362481
Ambapo majina yatakayopokelewa yatakabidhiwa kwenye Kamati ya Mchakato wa Kumpata Katibu Mkuu Shirikisho La Muziki Tanzania ambapo Kamati hiyo itaanza kukaa vikao vya kupitia walioomba kuanzia tarehe 18 April 2021.
Mwisho wa kutuma maombi hayo ni tarehe 17 April 2021.
Tafadhali washirikishe wadau wengine wote.
Imetolewa na Shirikisho la Muziki Tanzania.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment