Wateja kuwasiliana kwa gharama nafuu na kupata maudhui ya kiislamu kuhusu mfungo wa Ramadhan.
Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, leo imezindua ofa maalumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa wateja wake ili kuwawezesha kuwasiliana kwa gharama nafuu pamoja na kupata maaudhui mbalimbali yenye kuimarisha imani zao katika kipindi chote cha mwezi mtukufu.
Ofa hiyo inawapa wateja uhuru wa kuwasiliana zaidi pamoja na kupata taarifa muhimu kama vile nukuu mbalimbali za Koran takatifu pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala na ujumbe wa sauti utakaowakumbusha nyakati za iftar na nyakati za daku.
Akizindua ofa hiyo mjini Zanzibar, Mkuu wa Zantel Zanzibar Mohammed Mussa alisema ofa hiyo itawasaidia waumini wa dini ya kiislamu kuimarisha zaidi mahusiano baina ya ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki cha mfungo.
“Zantel inapenda kuwatakia waislamu wote mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan. Tunatambua mwezi huu ni muda muafaka wa kujenga mahusiano mazuri na ndugu, jamaa na marafiki hivyo ofa hii itahakikisha kwamba wateja wetu wanawasiliana bila mipaka na pia kuwapa taarifa zitakazosaidia kujiimarisha kiimani ili kufanikisha funga zao,” alisema Mussa.
Hivi karibuni Zantel ilizindua kampeni yake ijulikanayo kama “Pasua Anga Ki Zantel 4G” kwa lengo lakuwawezesha wateja kujua umuhimu wa mtandao wa 4G katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.Katika mwezi huu, waumini wanaweza kutumia mtandao wa 4G kwa kujiongezea maarifa juu ya chimbuko, swala mbalimbali na mambo yakufuata katika kipindi cha mfungo.
“Tunatambua kwamba huduma ya intaneti ni nyenzo muhimu katika kipindi hiki ambapo wengi watahitaji intaneti ili kuangalia vipindi mbalimbali vya dini, kujifunza na kubadilishana taarifa juu ya kipindi hiki cha Ramadhan.Kupitia vifurushi vyetu vya intaneti viliboreshwa wateja wanaweza kufanya mengi zaidi kwa kujiongezea maarifa kupitia mtandao wa 4G na kufanya kipindi hiki kuwa na thamani zaidi kwao,” alisema Mussa.
Naye, Mkuu wa Masoko wa Zantel-Zanzibar, Rukia Mtingwa alisema ofa hiyo itawazawadia wateja watakaojiunga na vifurushi vilivyoboreshwa zaidi vya siku, wiki na mwezi ambapo mbali na muda wa maongezi watajipatia nukuu za Koran takatifu pamoja na jumbe za kuwakumbusha muda wa swala tano.
“Tumeboresha zaidi vifurushi vyetu ili kuwapa wateja sababu zaidi za kuwasiliana msimu huu.Kwa wateja watakaojiunga kifurushi cha siku kwa Shilingi 1,000/- watajipatia dakika 150, SMS 100 pamoja na nukuu moja ya Koran, jumbe tano za kukumbusha muda wa swala,” alisema.
Vilevile, kwa kifurushi cha wiki cha Shilingi 2,000 mteja atapata dakika 250, SMS 200 huku kifurushi cha mwezi cha Shilingi 10,000/- atapata dakika 1,500, SMS 500 pamoja na nukuu mbalimbali za maandiko ya Koran takataifu, jumbe za kuwakumbusha muda wa kufuturu pamoja za kukumbusha muda wa swala.
Ili kujiunga na ofa hii mteja wa Zantel apige *149*15# na kuchagua namba 0 ambayo ni ofa ya Ramadhani na atajiunga na kifurushi anachohitaji.
Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa (Katikati) pamoja na Mkuu wa biashara wa Zantel, Aneth Muga (Kulia) na Meneja wa Masoko Rukia Mtingwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Ofa ya mwezi mtukufu wa Ramadhani inayowawezesha wateja kuwasiliana zaidi na kupata maudhui ya kiislamu kama nukuu za Quran tukufu na jumbe za kuwakumbusha wakati wa swala ili kuwawezesha kufanikisha funga zao.
Meneja Masoko wa Zantel-Zanzibar, Bi.Rukia Iddi Mtingwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofay a mwezi mtukufu wa Ramadhani inayowapa wateja uhuru wa kusaliana zaidi pamoja na maudhui ya kiislamu kama nukuu za Koran takatifu na jumbe za kuwakumbusha wakati wa swala ili kuwawezesha waislamu kufanikisha funga zao.Kushoto ni Mkuu wa Zantel-Zanzibar Mohammed Khamis Mussa.
Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohammed Khamis Mussa akizungumza wakati wa uzinduzi wa ofa ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ya Zantel inayowapa wateja uhuru wa kuwasiliana zaidi pamoja na maudhui ya Kiislam kama nukuu za Quran Tukufu na jumbe za kuwakumbusha wakati wa swala ili kuwawezesha waislamu kufanikisha funga zao.Kulia ni Meneja Masoko wa Zantel-Zanzibar Rukia Mtingwa
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment