TCCIA yanogesha sekta ya utalii jiji la Arusha | Tarimo Blog

Na Woinde Shizza , michuzi Tv
CHAMA Cha wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima mkoa wa Arusha (TCCIA) kwa kushirikiana na halmashauri ya jiji la Arusha kimeanzisha mpango wa kuotesha miti katika jiji la Arusha kwa lengo la kuboresha manzari ya jiji hilo na kuibua vivutio vya utalii vitakavyosaidia kuboresha sekta ya utalii.

Akiongea na vyombo vya habari leo wakati wa kuotesha miti 100 katika bustani tengefu ya mto Them (Themi Living Garden ) Ofisa la TCCIA, Charles Makoi alisema mpango huo unalenga kuotesha miti 20,000 katika kipindi Cha mwaka huu 2021.

Alisema chama hicho kimewekeza katika masuala ya utunzaji wa mazingira kwa kuimarisha sekta ya utalii na kuboresha masoko katikati ya jiji la Arusha.

Alisema mpango huu umeanza mwaka jana kwa kupanda miti 20,000 katika maeneo yaliyoathiriwa na ukame likiwemo la Muriet kwa Morombo.

Kwa upande wake Afisa mazingira na utalii jiji la Arusha, Maico Ndaisaba alisema mpango wa uoteshaji miti katika jiji la Arusha unalenga kuimarisha vivutio la utalii katikati yanjiji la Arusha.

Alisema mpango wa upandaji miti umeanza katika kata mbalimbali za jiji la Arusha na kwamba hadi Sasa wameotesha miti 15,000 katika kata za Muriet, Terat na Olmot na leo wamehitinisha zoezi hilo kwa kupanda miti 100 katika bustani ya Themi.

"Tunawashukuru Sana TCCIA wamekuwa wadau wakubwa wa utunzani wa mazingira na leo tunahitinisha zoezi la upandaji miti kwa kuotesha miti 100 katika bustani ya them ambayo imekuwa maarufu kwa utalii." Alisema

Ameongeza kuwa wameweka lengo la kuotesha miti 150,000 katika kata zilizokuwa pembezoni mwa jiji la Arusha zilizoathiriwa na ukame na kuwataka wadau wengine wa mazingira kujitokeza ili kubotesha mazingira ya jiji la Arusha ambalo ni kitovu Cha utalii.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2