Marium Mtumbuka (29) mkazi wa Jijini Ilala Mkoa wa Dar es Salaam akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo mara baada ya kusomewa mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya.
Katikati aliyeshika Karatasi, Hamis Awadhi (44) akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kusomewa mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevyaNa Karama Kenyunko Michuzi TV
MWANAMAMA Marium Mtumbuka (29) mkazi wa Jijini Ilala Mkoa wa Dar es Salaam na mwenzake Hamis Awadhi (44), wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya mahakimu wawili tofauti wakikabaliwa na tuhuma za kusafirisha zaidi ya kilogramu 13.15 za dawa za kulevya aina ya Heroin.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Faraja Ngukah mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Yusto Lubiroga imedai kuwa, Aprili 2, 2021 huko uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, uliopo Jijini Ilala Mkoa wa Dar es Salaam mshtakiwa Marium alikutwa akisafirisha Kg 6.65 za dawa za kulevya aina ya Heroin.
Aidha imedaiwa na wakili wa serikali, Ester Martin mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Kassian Matembele kuwa, siku na mahali hapo mshtakiwa Awadhi alikutwa akisafirisha kg 6.75 za dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Hata hivyo washtakiwa wote kwa nyakati tofauti hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida kusikilizwa mahakama Kuu kitengo cha mafisadi.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika hizo bado haujakamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 27.2021 washtakiwa wamerudishwa rumande.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment