Barrick kinara tuzo ya Usalama na Afya mahali pa kazi | Tarimo Blog
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Kazi, Ajira,Vijana na Walemavu,Jenista Mhagama akikabidhi kikombe kwa Meneja Usalama wa mgodi wa Barrick wa Bulyangulu, Dr. Kudra Said Mfaume, kwa niaba ya Barrick baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika kundi la migodi.Hafla ya kukabidhi tuzo ilifanyika wakati wa kilele cha maoinyesho ya wiki ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi yaliyoandaliwa na OSHA jijini Mwanza
Kampuni ya kuchimba madini ya Barrick Gold Corporation , imeshinda tuzo ya nafasi ya kwanza ya Usalama na Afya Mahala pa kazi kwa mwaka huu kwa upande wa sekta ya madini.
Tuzo hiyo inayotolewa na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa kazi Nchini (OSHA) imetolewa wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi Duniani ambayo kitaifa ilifanyika jijini Mwanza.
Kwa ushindi huo Barrick , imedhihirisha jinsi ambavyo Timu Moja Yenye Lengo Moja inavyoweza kuleta matokeo chanya kutokana na kuibuka mshindi wa kwanza
Taarifa kutoka Barrick , imeeleza kuwa ushindi wa tuzo hiyo iliyokabidhiwa kwa kampuni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge,kazi,Ajira na Walemavu , Mh.Jenista Mhagama, ni matokeo ya juhudi za makusudi ambazo kampuni imekuwa ikizitekeleza katika kulinda, kuhamasisha na kuimarisha usalama na Afya kwa wafanyakazi wake, wakandarasi na wadau mbalimbali inaoshirikiana nao.
Meneja wa masuala ya jamii wa kampuni ya Barrick ,Mary Lupamba, (kushoto) akitoa maelezo kuhusiana na kampuni inavyozingatia Usalama na Afya mahali pa kazi kwa Waziri Jenesta Mhagama, wakati alipotembelea banda la maonyesho la kampuni hiyo.Barrick iliibuka mshindi wa kwanza katika kundi la viwanda.
Kampuni imewashukuru wafanyakazi wake,wakandarasi na wadau wote kwa kuunga mkono sera, mikakati na miongozo yake inayolenga kuhimizana na kukumbushana umuhimu wa kuzingatia bila shuruti usalama na afya ya kila mmoja wakati anapotimiza majukumu yake, bila hivyo mafanikio haya ya ushindi yasingepatikana.
Mbali na ushindi huu mkubwa, kampuni imejiwekea lengo la uhakikisha kanuni za usalama zinatekelezwa ipasavyo katika maeneo yake yote ya kazi kufikia viwango vya kimataifa
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment