Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi akifungua mafunzo ya kuwaandaa wanafunzi wa mwaka wa mwaka wa kwanza namna ya kuingia katika soko la ajira leo mkoani Dar es Slaaam.
Mlezi wa wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es salaam -Tegeta, Zitta Mnyanyi, akizungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza wakati wa mafunzo ya kujiandaa na na soko la ajira. Mafunzo hayo yamefanyika Tegeta kwa wanafunzi wa degree ya kwanza.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam- Tegeta wakiwa katika mafunzo hayo yaliyotolewa na CV People Tanzania.
Afisa Rasilimaliwatu wa Kampuni ya CV People Tanzania, Noemi Mseven, akitoa mafunzo ya namna ya kuandika CV kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam-Tegeta.
Rais wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Festo Karoli, akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho wakati wa mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na CV People Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CV People, Naike Moshi, akitoa mada wakati wa mafunzo ya kuwaandaa wanafunzi wa mwaka wa kwanza namna ya kuingia katika soko la ajira.
CHUO Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam-Tegeta watoa mafunzo kwaajili ya wanafunzi wa chuo hicho kujiandaa kwaajili ya kuendana na soko la ajira mara aada ya kumaliza masomo yao.
Aidha Prof. Ngowi amesema kuwa mafunzo hayo sio ya mwisho, mafunzo hayo yatakuwa na mwendelezo kwani wataalika watu na makampuni mengine mengi ili kutoa mafunzo wanafunzi hao.
"Nyie wanafunzi wa awamu ya kwanza nataka muwe wazuri katika soko la ajira la dunia ndio maana tunaalika taasisi mbalimbali waje kutoa mafunzo mbalimbali kwenu." Amesema Profesa Ngowi
"Hata amesema kuwa mwanachuo anaweza kuwa na Maksi nzuri lakini kama hawana ujuzi wa namna a kuandika barua ya kazi, jinsi ya kujiandaa katika mahojiano ya kazi hiyo ni kazi bure kama watashindwa kuendana na soko la ajira la duniA ndio maana amewaalika kampuni ya CV People Tanzania." Amesema Prof. Ngowi
Licha ya hayo Prefesa Ngowi amewashukuru CV People Tanzania kwa kufika chuoni hapo kwaajili ya kutoa mafunzo kwa wanachuo ambao wanasoma ndaki ya Dar Es Salaam- Tegeta.
Mkurugenzi Mkuu wa CV People, Naike Moshi amewaasa wanachuo hao kuwa na mahusiano mazuri na watu wanaowazunguka kwani hawajui ni nani atakayewasaidia katika harakati zao za kutafuta kazi.
kwa upande wa Afisa Rasilimali watu wa CV People Tanzania, Noemi Mseven akizungumza wakati wa kutoa mafunzo ya uandishi wa barua ya kazi, wasifu wa masomo na ujuzi (CV) pamoja na mahojiano ya kazi (interview) amesema kuwa uandikazi mzuri wa barua ya kazi pamoja na CV unasaidia sana kwani inaonesha dahili mwombaji wa kazi anajua ni nini ataka katika nafasi ya kazi iliyotangazwa.
Kwaupande wa Mmoja ya wanafunzi amewashukuru CV People Tanzania kwa kuwapa mafunzo hayo kwani yatawasaidia katika harakati za kuandika barua za kuomba kujitolea na kuomba kazi mahali ambapo wanahitaji mfanyakazi.
"Ninawashukuru sana mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwa sasa tupo mwaka wa kwanza tutaanza kujiandaa mapema."
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment