Kampuni ya Nabaki Afrika Ltd, ambayo ni moja ya makampuni yanayoongoza katika usambazaji na uuzaji wa bidhaa bora za ujenzi nchini, imezindua kampeni maalumu ya uhamasishaji inayojulikana kama “IPS NI BOMBA” yenye lengo la kutangaza mabomba ya maji safi yenye ubora.
Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Bw.Vatsal Shah alisema bidhaa hii imekuwepo sokoni tangu mwaka 2000 na ilizinduliwa chini ya kampeni ijulikanayo kama “IPS
IPO” huku akisisitiza kuwa IPS ni moja ya bidhaa zinazouza mno tangu kuzinduliwa kwake katika soko la Tanzania.
Bw. Shah alisema hii imesababisha mabomba yoyote yenye rangi ya brown katika soko la Tanzania kuitwa “IPS.”
“Hii ni moja ya bidhaa bora katika soko letu na kampeni hii ya uhamasishaji inalenga pia kuwawezesha watanzania kutofautisha bidhaa halisi ya IPS na ambayo sio halisi,” alisema.
“Ni muda mwafaka sasa kwa watanzania kununua bidhaa zenye ubora kama IPS ambayo inatengenezwa nchini Argentina na ina waranti ya miaka 50 kwa sababu ya ubora wake,” alisema.
Alibainisha kuwa IPS ni bomba pekee lenye waranti ya miaka 50, ikiwa imetengenezwa kwa ubora wa kimataifa na kuipa uwezo wa kuhimili presha kubwa ya maji, chumvi na kemikali pamoja na kuhifadhi joto au baridi kwenye bomba na pia IPS ni bomba salama na linaweza kutumika kwa matumizi yote yanyumbani na viwandani
Kwa mujibu wa Bw. Shah, bomba la IPS imetengenezwa katika vipimo sahihi ambavyo huwapa mafundiwakati mwepesi kwani halivujishi maji.
“Bomba la IPS lina rangi ya brown na mstari wa kijani, maandishi meupe na ili kujua bomba halisi utaonamaandishi ya kispaniora - CALIDAD IPS.
Alisema bomba za IPS zina safu nne ambazo zinafanya bomba hili liwe bora kuliko mabomba mengine sokoni na safu hizi husaidia kulinda bomba dhidi ya miyonzi ya jua, kuweka maji safi na safu moja husaidia kuunga bomba vizuri ili maji yasivuje na pia ina plastiki ngumu ambayo haichakai hivi kuifanya bomba iwe imara kabisa.
Alisema bomba za IPS na viungio vyake zinapatikana Nabaki Afrika Ltd na katika maduka ya wasamba-zaji wake walioidhinishwa nchi nzima.
“Tunatoa wito kwa watanzania kuzingatia ubora kwani hii itawapa thamani ya fedha wanayostahili nakuwaondolea usumbufu wa kubadilisha bomba kila mara,” alisema.
Nabaki Afrika Ltd, ambayo ni moja ya makampuni yanayoongoza katika usambazaji na uuzaji wa bidhaazilizotengenezwa nchini na nje ya nchi, ina matawi Kariakoo, Masaki, Boko and Mikocheni (MakaoMakuu) Jijini Dar es Salaam. Kwa Arusha wanapatikana Nanenane Business Park, Njiro.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment