Na Woinde Shizza ,Michuzi Tv
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Hassan Kimanta ameuwagiza uongozi wa Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro (NCAA) kuhamisha Kaya 45 za watu zilizohamishwa awamu ya kwanza kwenda katika Kijiji cha Jema na wakarudi tena hifadhini.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Jema Kata ya Oldonyosambu Wilayani Ngorongoro kwenye mkutano wa hadhara baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu iliyopo katika Kijiji hicho.
Kimanta amesema, watu waliopo katika Kaya hizo 45 walishalipwa shahiki zao zote na baadhi yao waliuza maeneo waliyogawiwa na serikali katika Kijiji cha Jema na kurudi tena hifadhini.
Amesema, Kaya hizo 45 zinatakiwa kurudi Kijiji cha Jema ndani ya siku 30 baada ya kutolewa tangazo la kuhamu.
Serikali imewekeza zaidi ya bilioni 4 katika Kijiji cha Jema kwa kuleta miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Maji, Shule na Zahanati.
Naibu Kamishina wa uwifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro Christopher Timbuka amesema, jumla ya Kaya 113 zilihamishwa kati ya mwaka 2006 hadi 2021 na Kaya 45 zilirudi tena eneo la hifadhi.
Amesema kaya hizo ndizo zinatakiwa kutoka katika eneo la hifadhi na kurudi katika Kijiji cha Jema au eneo lingine mbali watakalo chagua.
Kamishina Timbuka amesema Mamlaka ilinunua jumla ya hekari 13,000 kwa ajili ya kuwagawia watu wote waliotakiwa kuhama eneo la hifadhi.RC Kimanta amefanya ziara ya siku 2 katika Kijiji cha Jema Wilaya ya Ngorongoro na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Maji na Shule.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Iddi Kimanta akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Jema Kata ya Oldonyosambu Wilayani Ngorongoro kwenye mkutano wa hadhara baada ya kufanya ziara ya kukagua miundombinu iliyopo katika Kijiji hicho(picha na Woinde Shizza , ARUSHA)
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment