Mbunge wa Wanging'ombe aahidi kufanya makubwa kata inayoongozwa na Chadema | Tarimo Blog

 Na Amiri Kilagalila,NJOMBE

Naibu waziri wa nchi,ofisi ya Rais,tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) ambaye ni mbunge wa jimbo la Wanging'ombe mkoani Njombe Dkt,Festo Dugange amesema licha ya kuwa kata ya Uhenga inaongozwa na diwani wa Chama cha upinzani (CHADEMA), bado ataendelea kuhakikisha shughuli za kimaendeleo zinaendelea kutekelezwa kwa kasi kubwa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika kijiji hicho cha uhenga mbuge huyo Dkt,Dugange amewahakikishia wananchi kuwa atatekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo bila upendeleo.

Aidha Dkt Dugange amesema kuwa ataendelea kushirikiana na diwani aliyepo kwa sasa madalakani kwa sasa kwa kuwa lengo lao kwa sasa ni kuwahudumia wananchi kwa kuwapelekea maendeleo.

Awali akizungumza katibu wa umoja wa wanawake wilayani Wanging'ombe (UWT) Fatma Ngole amewataka wananchi kuwapuuza baadhi ya watu wanaodai kuwa Uhenga haitatekelezewa miradi ya kimaendeleo kwa kuwa imechagua kiongozi kutoka chama cha upizani cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Kwa upande wake diwani wa kata hiyo ya Halfan Kawambwa amewashukuru viongozi wa wilaya hiyo kwa ushirikiano wanaotoa kwake na kueleza kuwa kwa sasa hakuna haja ya kuendeleza mambo ya kisiasa kwa kuwa uchaguzi umeshapita.

Kata ya Uhenga ni kata pekee kati ya kata 21 inayoongozwa na upinzani huku kata zingine zikiongozwa na Chama cha Mapinduzi.

 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2