Raisa Said,Pangani.
SHUGHULI za ulinzi wa rasilimali za bahari Wilayani hapa zinatarajiwa kuimarika zaidi baada ofisi ya Kikundi cha Ulinzi Shirikishi Beach - Management Unit (BMU) Kipumbwi Wilayani Pangani Mkoani Tanga kuzinduliwa na mwenge wa Uhuru
Ofisi hiyo ya kisasa imezinduliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Maalum wa uhuru Kitaifa mwaka 2021 Josephine Mwambashi baada ya kakamilika kwa asilimia 98.
Akizungumza kuhusu mradi huo unaotekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Uvuvi kupitia Mradi wa SWIOfish Tanzania Bara unafadhiliwa na Banki ya Dunia Mwambashi alisema ni matarajio kuwa shughuli za ulinzi zitaimarika.
Akisoma taarifa baada ya Mwenge wa uhuru kufika katika Ofisi hiyo Kaimu Afisa Mifugo na Uvuvi Aristariki Kimario Alisema kuwa mradi huo ulioanza kutekelezwa July 28 mwaka jana ulitakiwa kukamilika Desemba 3 mwaka jana nakwamba umegharimu sh. Million 151.5 ikiwa ni pamoja na ongezeko la thamani.
Alisema kuwa mradi huo utaimarisha usimamizi wa rasilimali za Uvuvi kwa kujenga miundombinu, kusogeza zaidi usimamizi wa rasilimali ngazi ya Jamii yani BMU ,kuimarisha mahusiano Kati ya wavuvi , serikali na jamii ambayo inasimamia shughuli za uvuvi na kusogeza huduma ya wagani kwa kuwapatia sehemu nzuri ya kufanyia kazi na kusimamia rasilimali za uvuvi kwa ujumla.
Hata hivyo alisema kuwa katika kuhakikisha ubora wa kazi unazingatiwa viwango na vigezo uhakiki wa mara kwa Mara wa ubora wa viwango ,mazingira na usalama kazini ulifanyika.
Waziri wa Maji ambaye ni Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Aweso alisema wao kama pangani hawakujaliwa kupata dhahabu lakini wamejaliwa kuwa na bahari ambapo aliongeza kuwa wanaishukuru serikali kwa kuwapatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo la ofisi kwa ajili ya BMU.
Aweso alisema licha ya kukamilika kwa jengo hilo lakini halina samani za ndani hivyo aliwataka wakae pamoja ili waangalie namna ya kupata samani hizo za ofisi
Hata hivyo Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa alisema kuwa ameridhishwa na ujenzi huo nakwamba ubora wa jengo unaendana na thamani gharama halisi za mradi huo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment