Na John Nditi, Morogoro
SHIRIKA la Kimataifa lisilo la Kiserikali la Sightsavers kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa Morogoro wameezisha utekelezaji wa mpango wa kutokomeza upofu na utoaji wa huduma ya urekebishaji wa vikope kwa wananchi wa halmashauri za wilaya ya Morogoro na Gairo.
Utakelezaji wa mpango huo ulianza Mei mwaka huu (2021) na kutarajiwa kufikia tamati Juanuri 2023, unafadhiliwa na Sightsavers kwa kutengewa fedha kiasi cha sh milioni 328 .
Meneja wa Mradi wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele na msimamizi wa mradi wa kutokomeza vikope kupitia program ya Step Safe , Peter Kuvumbi alisema hayo mjini Morogoro wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa mpango huo kwa halmashauri hizo mbili.
Utekelezaji wa mpango huo ulinzinduliwa na Katibu Tawala wa mkoa huo , Mhandisi Emmanuel Kalobelo ulienda sambamba kukabishiwa kwa vifaa tiba na dawa vitakavyotumika katika uchunguzi na upasuaji wa macho kwa waathirika wa ugonjwa wa vikope kwa halmashauri ya wilaya ya Morogoro , na Gairo.
Alisema ,kupitia mpango huo utawahudumia watu wote wakataobainika na ugonjwa wa vikope kwenye halmashauri ya wiliaya ya Morogoro pamoja na wilaya ya Gairo.
“ Utekelezaji wa mpango huu unatokana na utafiti uliofanywa na Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto mwaka 2018 ambapo ulibaini kugundulika kwa wangonjwa 353 halamshauri ya wilaya ya Morogoro na wagonjwa 548 wilaya ya Gairo na leo ni mwaka 2021 huwenda wingine wameongezeka” alisema
Naye Mkurugenzi mkazi wa Sightsavers hapa nchini , Godwin Kabalika alisema , wamejipanga kuendelea mradi huo ulianzishwa licha ya rasilimali fedha kidogo inayopatikana .
Kabalika alisema ,lengo kubwa ni kuwasaidia wananchi wengi wenye matatizo macho ili waweze kupata huduma za matibabu karibu yao na hivyo kutokomeza ugonjwa wa trakoma unaosababisha upofu.
Alisema ,Shirika litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali na serikali ya mkoa huo kwa kufanya kila liwezekanalo ili kutokomeza upofu.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Kalobelo ,licha ya kulipongeza shirika hilo ,alitoa rai kwa wananchi na viongozi watakaoshiriki kutoa matibabu ya ugonjwa wa vikope kuwashirikisha viongozi wa maeneo husika.
Mhandisi Kalobelo alisema ,ushirikishaji kwa viongozi wa maeneo husika wakiwemo wenyeviti wa vijiji, vitongozi na viongozi wa kaya ni jambo la muhimu ili kupata mafanikio ya utekelezaji wa mradi huo .
“ Hawa wagonjwa wanaenda kutafutwa , lakini haiwezekani mtaalamu ukatoka mkoani , wilayani ukapata mgonjwa bila kuwashirikisha viongozi hawa , washirikisheni viongozi mbalimbali ni muhimu katika kupata mafanikio yetu” alisema Mhandisi Kalobelo.
Hata hivyo ,aliwataka wananchi kuweka mazingira katika hali ya usafi kwani ugonjwa wa vikope na kutumia maji safi na salama kwani kutokekana kwa mambo hayo kunachangia uwepo wa mazingira machafu na kusababisha wananchi kupatwa na vikope
Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Kalobelo akimkabidhi Mganga mkuu wa mkoa huo, Dk Kusirye Ukio , ( kulia) sehemu ya vifaa kwa ajili ya utoaji wa huduma ya urekebishaji wa vikope ( Trachoma ) vitakavyotumika kwenye halmashauri ya wilaya ya Morogoro pamoja na Gairo vilivyotolewa na Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la Sightsavers katika utekelezaji wa mradi Step Safe Trachoma uliaonza mwaka huu hadi 2023.
Katibu Tawala wa mkoa wa Morogoro, Mhandisi Emmanuel Kalobelo ,akikata utepe kuzindua kitabu cha mradi Step Safe Trachoma unaonza kutekelewa mwaka huu (2021) na kufikiwa tamati mwaka 2023 katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro pamoja na Gairo kupitia ufadhili wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la Sightsavers , ( kulia ) ni Mganga mkuu wa mkoa huo, Dk Kusirye Ukio .( Picha na John Nditi).
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment